HUU
ni msimu wa sikukuu! Juzi, tumesherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2014. Kwa nguvu za Mungu tutafika salama. Ndugu
zangu, hebu tutafakari vizuri kuhusu mwaka uliopita na kuangalia cha
maana tulichofanya kwa wenzi wetu. Tuliwaumiza au tuliwapa furaha? Je, kupitia kona hii matatizo yameondoka, yamepungua au yameongezeka?
Nimeandika mada nyingi ambazo zimewagusa watu wengi. Ujumbe wenu na
simu mlizopiga zinaonyesha jinsi kona hii inavyosomwa na watu wengi,
tena makini.
Kwa
vile tunakaribia kumaliza mwaka na kuanza mwingine mpya, basi napenda
kuwapa kazi ya kufanya utafiti kuhusiana na mwenendo mzima wa maisha
yenu ya kimapenzi. Huu ndiyo muda muafaka wa kujichambua mwenyewe
ulibeba vipi uhusiano ndani ya penzi lako.
Katika
muda wote kulikuwa na migongano, je, chanzo chake nini? Kama ni wewe
ni muda wako wa kujirekebisha ili usiwe chanzo cha matatizo ya kila
siku.
Ni
makosa mtu kurudia kosa moja kila mara, mwanadamu anayejitambua
hujifunza kupitia lile linalokemewa sana na mwenzake, japokuwa unapenda
kulifanya.
Sifa
kubwa ya mwanadamu ni kufikiri kabla ya kutenda, siku zote mapenzi ni
kusikilizana, kufarijiana na kubembelezana. Bila shaka mwaka huu
unaomalizika kuna mambo yalitokea hadi kufikia hatua ya kutishia
kuvunja ndoa au uhusiano wenu.
Mwaka unaisha, umekaa na kujiuliza tatizo nini? Umejichunguza na kujua labda wewe ndiye chanzo?
Mmeukaribisha mwaka, mmekaa kama wanandoa au wapenzi kumaliza tofauti zenu?
Kama
hamjakaa kujadili mwenendo mzima wa uhusiano wenu kwa mwaka mzima
hamjachelewa. Hebu kupitia makala haya kaeni chini na kuchambua
matatizo yote yaliyowakwaza sana.
Tafuteni sehemu tulivu ili kupata
nafasi ya kuzungumza kwa kujiamini. Sehemu hii haitakiwi mmoja kujiona
yupo juu ya mwenzake au ubishi kwa kile ambacho kimemgusa.
Mazungumzo
yenu yawe ya kirafiki, kosoaneni kwa sauti za kawaida, ondoeni jazba
kwani muda huo hauna nafasi. Uwe mwepesi kukubali kosa na kuomba
msamaha. Kwa vile nia yenu ni kujenga, hakikisheni yote yaliyowakwaza
mwaka uliopita hamyapi tena nafasi. Jiepusheni
kuwa chanzo cha maumivu ya wenzenu, umeamua huyo awe wako wa kufa na
kuzikana kwa nini muumizane? Sawa, mwanadamu ana upungufu, basi makosa
yako yasiwe mazoea kwa vile tu upo juu ya mwenzako.
Mapenzi hayaangalii cheo, fedha wala uzuri wa sura na umbile, bali kujitoa kwa ajili ya mwenzako.
Jutia makosa uliyofanya mwaka huu na uanze upya mwaka ujao.
Anza
mwaka ukiwa makini sana na kumfanya mpenzi wako asahau maumivu ya
mwaka jana. Muahidi mpenzi wako kuwa mwaka huu utakuwa sehemu ya furaha
yake ya kila siku, kama utakwenda tofauti basi utakuwa msaliti.
Kiapo
hiki si cha mtu mmoja bali kiwe cha wote. Kama kweli unayosema
yanatoka moyoni na kuwa tayari kutorudia yaliyomkwaza mwenzako mwaka huu
unaoishia, basi mwaka ujao utakuwa wa furaha na amani. Nakutakieni
mwaka mpya wenye mapenzi ya dhati, kila mmoja awe sehemu ya furaha ya
mwenzake.
No comments:
Post a Comment