Mtandao wa rushwa kwa baadhi ya mahakama nchini, umeelezwa kuwa moja kati ya changamoto na kikwazo kikubwa katika harakati za upatikanaji haki za wanawake.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa maonyesho ya
ukombozi wa mwanamke Afrika na duniani jana, Mwanzilishi wa Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Fatma Aloo alisema kesi
nyingi za vitendo vya unyanyasaji wanawake zinapofikishwa mahakamani
zimekuwa zikikwama kutokana na rushwa.
“Rushwa ni kikwazo kikubwa, lakini jambo la msingi
kwa jamii ni kuhakikisha elimu inatolewa kwa watoto wa kike ili kuibua
zaidi vitendo vya ukatili,” alisema Aloona kuongeza:
“Nafurahi kuona maonyesho haya yakifanyika nchini,
hiyo ni kwa sababu ya heshima kubwa tuliyonayo Tanzania katika harakati
za ukombozi.”
Naye Peirre Yves Ginet ambaye atahusika katika
maonyesho hayo yatakayofanyika viwanja vya Alliance Francaise, alisema
tangu mwaka 1998 hadi 2012 amezunguka mataifa 24 akipiga picha za
matukio ya wanawake ili kuonyesha uhalisia wa changamoto zinazokabili.
Pierre alisema mwanamke anakabiliwa na changamoto maeneo mbalimbali, hivyo jamii inatakiwa kuongeza kasi ya harakati.
Katika maonyesho hayo yanashirikisha Umoja wa Nchi
za Ulaya (EU), ubalozi wa Norway, Uswiz, Umoja wa Mataifa (UN) na
Ubalozi wa Ufaransa nchini.
Pia, Tanzania itapata fursa ya kujifunza na kukuza
mazingira ya harakati za kumkomboa mwanamke nchini. Tayari, mitandao
mbalimbali imekuwa ikiendesha harakati za kupinga ukatili wa jinsi,
kutokana na mila potofu.
No comments:
Post a Comment