Sunday, 19 May 2013

Mbunge wa Chadema Mbaroni kwa kuchochea vurugu Iringa...




WAKATI hali ikizidi kuwa tete Mkoani Iringa, kutokana na vurugu za wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga na Askari wa Jeshi la Polisi  ukizidi kupamba moto, Jeshi hilo linamshikilia Mbunge wa Chadema Peter Msigwa.
Waandishi wa habari  wakiwa katika aneo la tukio anaripoti kwamba Mbunge huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kuchochea na kusababisha vurugu hizo za wamachinga.
Vurugu hizo za Wamachinga na Polisi zilianza tangu asubuhi ya leo na kuilazimu Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wamachinga hao, waliokuwa wakijaribu kuandamana.

No comments:

Post a Comment