Tuesday 21 January 2014

MAPENZI MATAMU SANA....MDADA FAHAMU NJIA 18 ZA "KUMSHIKA" KIDUME YEYOTE ULIMWENGUNI...!

I was single once, but now i'm a wife and a mother. Nimekaa nikaona sio vibaya iwapo nta-share tips kadhaa zilizonisaidia kumuweka baba watoto sawa na mpaka leo hii sijawahi kuhisi wala kugundua kwamba anatoka nje ya ndoa yetu, japo matatizo ya hapa na pale hayakosekani ila tumedumu na bado tunaendelea na safari.
Unapokutana na mwanaume akakutongoza/mwanamke akakukubalia kuna uwezekano mkubwa kuwa amevutiwa na wewe kweli au kakutamani tu. Kitu ambacho watu hua wanasahau ni kwamba hata mtu aliyekutamani tu unaweza ukampa mwongozo/sababu mpaka mwenyewe akajikuta anakupenda kuliko ambavyo angeweza kutarajia kwamba angewahi kupenda. Ndio maana hata wale waitwao 'bad girls/boys' hua wanajikuta wamenaswa na kunasika at some point.

1. Usiigize.
Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/mazoea n.k

2. Don't move too fast/act desperate.
Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa wa mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo gani na mie?" "utanioa?" "Kanitambulishe/nataka nikakutambulishe." n.k Mpe nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa aina gani, je unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho hicho.

3.Don't be too demanding.
Huyo sio baba yako wala sio mume just yet, hivyo chochote atakachokufanyia kinatokana na yeye kutaka/kupenda kufanya hivyo na sio kwakulazimika. Haki hiyo hauna.

4. Kuwa na shukurani.
Learn to appreciate all that he does for you, that way ataona umuhimu wa hayo anayokufanyia, yawe makubwa au madogo.

5. Be real.
Badala ya kufika kwake na kuanza kushangaa anaishije bila ya mfanyakazi wa ndani huku ukitamba kuwa wewe huwezi, shangaa anawezaje weka nyumba yake katika hali nzuri mwenyewe bila ya msaada. Hii itaonyesha fika wewe utakua mke wa aina gani hapo baadae, kama ni wale wakukaa miguu juu huku wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au la.

6. Learn to cook if you don't know how to.
Waliosema "the way to a man's heart is through his stomach" hawakukosea. Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili kushiba wengi hua wanajali ladha. Hiyo ndio hua inawaongezea hamu ya kula na kuwarudisha nyumbani mapema pia kuwafanya wakumiss pale inaposhindikana kula chakula chako . Kwakumwonyesha mwanaume kwamba hata tumbo lake unaweza kuliridhisha unamwongezea sababu za kukuweka kwenye maisha yake.

7. Mheshimu.
Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba haheshimiki.

8. Kuwa ngao yake.
Inapotokea anakumbwa na matatizo yoyote yale onyesha utayari wa wewe kuwa pamoja naye kwa hali na mali mpaka yatakapoisha. Pia usikose kumjali kumpa moyo pale unapoona inahitajika.

9. Kuwa muwazi.
Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa moja yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema ili aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la.

10. Usiwe na chuki.
Kikifika kipindi cha yeye kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake onyesha ushirikiano. Usionyeshe chuki wala kujiona kana kwamba wewe ndio wewe.

11. Give your all.
Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na usiwe mvivu.

12.Pendeza.
Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje hata ndani pia. Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu mavazi 
yako.

13. Onyesha interest kwa yale ayapendayo yeye.
Usiwe mbinafsi kila siku unataka kusikilizwa wewe tu na story/mambo utakayo wewe. Uliza/jua kuhusu yale anayopenda yeye mf. mpira/siasa.

14.Kuwa mtulivu.
Usiwe mtu ambae kila saa simu yako inapigwa pigwa na wanaume wasio ndugu wala marafiki wakaribu na wanaoeleweka. Discpline ni muhimu sana.

15.Usimzonge.
Usiwe mmoja wa wale watu wanaofuatilia wenzi wao masaa yote wanapokuwa hawapo pamoja. Mpe nafasi ya kuwa na marafiki zake bila kuhitaji kuzima simu ama ku-ignore simu/text zako.

16. Mfurahishe/chekeshe.
Joke around sio muda wote yeye ndio awe wakukufurahisha wewe.

17. Jifunze kusamehe.
Mambo madogo madogo yanapoombewa msamaha samehe na uache yapite.

18. Mshirikishe Mungu wako.
Ukishaona kwamba huyo ndie basi mshirikishe yule unayemwamini ili upate mwongozo wa kiroho.

2 comments:

  1. Unamshirikisha MUNGU kwanza sio Mungu anashirikishwa mwishoni kumbuka MUNGU asipoilinda nyumba yako wailindao wafanya kazi bure

    ReplyDelete
  2. Apo lazima nishikwe ila umbo la duara kwa mwa mwanamke na kudumisha UAFRIKA wake ndo mpango mzima

    ReplyDelete