Rangi
inaweza kuelezea hisia zetu, matendo yetu na hata namna tunavyoweza
kuvichukulia vitu katika masuala mbalimbali ikiwemo watu, vitu Fulani
na hata mawazo yetu. Mengi yameandikwa na kutolewa elimu juu ya rangi
na namna yanavyogusa maisha yetu ya kila siku.
Rangi
ziko kila kona katika maisha yetu zinatuzunguka.Tunaziona wakati wote,
ingawa wengi wetu hatujui rangi hizo zina matokeo gani katika maisha
yetu ya kila siku. Matokeo ya kuwa na rangi nyingi katika mazingira yetu
kwa kawaida hatufahamu. Mara nyingine tunapata hisia zisizo rahisi
katika baadhi ya vyumba unapoingia au unapata faraja na burudisho kiaina
Fulani,lakini sisi tunaita hilo TABIA. ”Rangi za Tabia” ndizo
tunazoweza kusema zinatuzunguka
Wengi
wetu huamini kuwa Rangi ni Nguvu na uwezo, na kwamba rangi za vito vya
thamani ni vyenye nguvu zaidi na kwamba vito hivyo vya rangi huwa na
nguvu maalum .
Kutokana na hivyo basi, hebu tuangalie maana halisi ya rangi zifuatazo na nguvu zilizonazo katika maisha yetu ya kila siku.
NYEKUNDU HUMAANISHA: VITENDO, KUJIAMINI ,UJASIRI NA KUIMARIKA.(VITALITY).
Rangi
nyekundu ni rangi ya kuvutia kuliko zote. Rangi hii huchaguliwa zaidi
na watu waongeaji zaidi na ni rangi inayopendwa zaidi na wanaume.
Ingawa kwa upande hasa kwa maana nyingine ni rangi inayotafsiriwa kuwa
ni ya watu wenye HASIRA au KISARANI.
Lakini
nchini China, Rangi nyekundu huchukuliwa kama Rangi ya mafanikio na
Furaha.Mabibi harusi huvishwa Rangi nyekundi na milango ya watu wa china
hupakwa rangi Nyekundu. Rangi nyekundu pia hutumika Kama rangi ya siku
ya Jumanne.
Maua
ya Rose mekundu nayo humaanisha mapenzi ya dhati.Iwapo utavaa pete
yenye kito cha Ruby ambayo ni nyekundu inatakiwa uvae mkono wa kushoto.
Rangi nyekundu ni rangi ya sayari ya MARS, na sayari hii inajuliakana
kama sayari ya MUNGU wa Vita.
UVAAPO RANGI NYEKUNDU
Enzi
hizo ulipokuwa ukivaa nyekundu ilikuwa ukimaanisha kwamba
unajitambulisha kwa jamii kwamba wewe ni mtu mwenye msimamo na unayeweza
lolote. Pia ilionyesha kama njia ya kuongeza kujiamini kwako iwapo
unahudhuria sherehe au tukio la mahojiano iwapo unajihisi kutokuwa na
uhakika na ufanyalo.
Na
iwapo mwanamke atakuwa amevaa nguo nyekundu ilikuwa ni kielelezo cha
kawaida kuwa tayari mwanamke huyo ameshajiingiza kwenye mahusiano ya
kimapenzi.
RANGI YA PINK INAMAANISHA: UPENDO NA UZURI.
Rangi ya Pink ni rangi ya upendo
usio na mipaka. Pink ni rangi ya ukimya. Wapenzi wa Urembo hupendelea
rangi ya Pink. Ua la pink maana yake ni “SINTAKUSAHAU KAMWE “.
NGUVU YA RANGI YA PINK
Pink
ni mchanganyiko wa rangi nyekundu na nyeupe.Na kiwango cha nguvu ya
pink inategemeana na ni kiasi gani cha wekundu kilichopo. Ingawa nyeupe
ni muhimu kwa ajili kukamilisha,huku nyekundu ikisaidia kutimiza umuhimu
huo.
Rangi
ya PINK hujumisha nguvu hizo. Urembo uliosheheni rangi ya PINK
iliyokoza kama rangi ya magenta inaelezea kusawazisha mambo yasiyokaa
vema na vurugu.Baadhi ya wafungwa hutumia rangi ya PINK iliyokoza
kuondoa tabia za ukatili.
Rangi ya PINK hutumika kuelezea hisa za kujali, upole,kujijali na kupenda sambamba na kukubalika.
KUVAA RANGI YA PINK
Vaa rangi ya pink iwapo unataka kujiwakilisha mwenyewe kama mtu wa amani ,mpole ambaye hatishiki na chochote.
RANGI YA KIJANI HUMAANISHA: MAISHA, UHALISIA NAUZAO NA UTU.
Rangi
ya kijani ni rangi ya asilia, maisha na uzao.. Majani ya kijani ndiyo
rangi iliyotulia zaidi. Rangi ya kijani inamaanisha kujiheshimu na utu.
Rangi ya kijani ni rangi ya uwiano.
Pia
inamaanisha kujifunza,kukua na utulivu.Rangi ya kijani ni rangi salama
,Kama hujui rangi ya kutumia sehemu yoyote basi tumia rangi ya kijani.
Rangi
ya kijani inapendwa na watu walio na maisha yenye uwiano bora kabisa.
Rangi ya kijani inamaanisha uponyaji mkuu na nguvu ya maisha. Na mara
kwa mara husimama kama ishara ya PESA.Inaaminika pia rangi ya kijani
huponya macho.
Wamisri
walivaa rangi za kijani katika nyusi kama wacha.Ingawa kwa sasa bado
wanatumia urembo wa kijani katika macho. Unatakiwa kula vyakula vya
kijani ambavyo ndivyo vyakula bora kwa afya.
Siku ya Ijumaa ndiyo siku ya Rangi ya Kijani kwa wale wanaoamini hivyo.Kito cha kijani ndicho kito kitakatifu kwa watu wa Asia.
KIJANI NI NGUVU
Rangi
ya kijani hujumuisha nguvu za asili,ukuaji na matamanio ya kupanuka au
kukua.Uwiano wa usawa na mpangilio vinapatikana katika rangi ya
kijani.Mabadiliko na mapitio ni muhimu katika ukuaji,hivyo ili uwezo huo
uendelee kusalia pia ni sehemu ya nguvu ya kijani kuwepo.
UVAAJI WA RANGI YA KIJANI
Vaa
rangi ya kijani pale unapotaka kushinda hisia za kuchanganyikiwa. Rangi
ya kijani tunaweza kusema ni rangi ya ustawi,uwiano na utulivu.Ni rangi
ya Mahusiano yenye Afya.
RANGI YA CHUNGWA INAMAANISHA: USTAWI NA UVUMILIVU
Rangi
ya chungwa ni rangi yenye nguvu.Ni moja kati ya rangi zenye uponyaji.
Inasemekana huongeza matamanio katika chakula.Pia husisimua furaha na
ubunifu.
Rangi
ya Chungwa inamaanisha Ustawi na Uvumilivu.Watu ambao wanapenda rangi
hii mara nyingi hutafsiriwa kuwa mawazo yao ni ya kweli na
yanayokubalika.Rangi ya mwanamke ya bahati ni rangi ya Chungwa.Ni imani
iliyopo kwa wengi kuwa iwapo unataka mabadiliko Fulani katika maisha
yako, CHOMA mshumaa wa rangi ya chungwa kwa Usiku SABA na itatokea.
NGUVU YA RANGI YA CHUNGWA
Wakati
rangi nyekundi ikihusishwa na joto kali, rangi ya chungwa inahusishwa
na uvuguvugu wa jua. Rangi ya mabadiliko ya kweli ni rangi ya chungwa
ambayo inatoa uwezo wa kufikiri kuliko mlipuko wa ile Nyekundu. Kupenda
kufahamu mambo ndiyo kichocheo cha tabia ya rangi ya chungwa, na ambayo
huleta matokeo ya kutambua mambo mapya.
KUVAA RANGI YA CHUNGWA
Kuvaa
vitu vya rangi ya chungwa wakati wa msongo wa mawazo,au hofu huweza
kusaidia kusawazisha hali iliyonayo kwa wakati huo.Inaweza kuleta hali
ya kukubaliana na mawazo hayo mapya huku ukiwa mwenye furaha na mvumbuzi
pamoja na kuwa kiongozi wa kutambua na kubuni.
RANGI YA BLUU HUMAANISHA: UJANA, MUUMINI WA KIROHO, UKWELI NA AMANI.
Rangi ya bluu ni rangi
iliyotulia zaidi , ni rangi ya Wingu, bahari, usingizi, na nyota. Watu
wa kale wa Misri walitumia rangi hii wakiita lapis lazuli kama
kiwakilishi cha mbinguni. Pia kwa wale waumini wa katoliki hutumia rangi
ya bluu kama kiwakilishi cha Bikira Maria.
Rangi halisi ya Bluu ni rangi ya
matamanio,ukweli na kiroho. Rangi ya Bluu mara nyingi ni rangi ambayo
huchaguliwa sana na watu wenye misimamo mikali. Ingawa kwa wengine rangi
hii ni rangi ya kutuliza..
Mara nyingi Rangi ya Bluu
hupendeza zaidi kwa matumizi ya nyumbani hususani kwa watoto wachanga,
pia ni rangi ya kubebembeleza ambayo ni nzuri unapochagua nguo ya
kulalia(pajamas).Rangi ya bluu ya kukoza sana ni rangi ya ukweli na
msimamo kiasi. Rangi ya bluu katika kona ya mboni inamaanisha kuwa
urafiki wako ni muhimu sana kwangu.Jumatano ndiyo rangi ya Bluu.
Kwa wale wanaoamini uvaaji wa vito vya thamani , uvaapo kito cha rangi ya bluu hukupa hisia za utulivu .
Huku rangi ya bluu bahari maarufu
kama (AQUA BLUE) yenyewe ni rangi inayoelezewa kuwa ya watu wenye fikra
za hali ya juu katika mambo muhimu.
NGUVU YA RANGI YA BLUU
Rangi
ya bluu hukupa hisia za umbali.Wasanii wa michoro hutumia rangi hii
katika kuonyesha umuhimu wa muonekano wa jambo.Na hili ni muhimu katika
kuonyesha uelewa wa nguvu ya rangi ya bluu.–inaturuhusu sisi kuangalia
mbele na kuongeza jitihada katika matarajio yetu ya baadaye.Inajumuisha
msisimko baridi ambao unasaidia katika mawasiliano.
Iwapo
rangi ya bluu itatumika, nguvu ya msisimko wake unaweza saidia kufungua
sehemu iliyofungika.Tumia rangi ya bluu iwapo unahitaji kupunguza na
itakusaidia katika kuongoza hisia za mawasiliano na utulivu.
KUVAA BLUU
Vaa
bluu iliyokoza kwa ajili ya uimara, kutuliza hisia zenye msimamo
usiobadilika.Pia mapambo yote ya macho ya rangi ya bluu husaidia
kurahisisha mawasiliano, iwapo ni kwako mwenyewe au kwa wengine.
Tumia karatasi ya bluu iwapo unataka msaada wa kukumbuka taarifa utayoiandaa au hotuba.
RANGI YA ZAMBARAU AU HUDHURUNGI HUMAANISHA: UAMINIFU NA MIUJIZA AU MAAJABU.
Rangi
ya Hudhurungi au Zambarau ni rangi za kufanya uamuzi mzuri.Ni rangi ya
watu wanaotafuta kukidhi mahitaji yao ya kiroho.Inasemekana kuwa iwapo
utazungukwa na mandhari iliyoshehena rangi ya zambarau unatarajiwa kuwa
mwenye utulivu wa akili au amani ya roho.Rangi hii ni nzuri kwaajili ya
Kufanya maombi ya utulivu.
Rangi
ya zambarau imekuwa ikitumika katika kumaanisha miujiza na
maajabu,sambamba na kutumika kama ishara ya uaminifu.Rangi hii ambayo ni
mchanganyiko wa rangi nyekundu na bluu, rangi ambazo hupendeza na
kuvutia zaidi,imeifanya rangi hii ya zambarau kuwa rangi ya kufikirika
zaidi.Watoto wengi hupenda rangi ya zambarau, na pia ni rangi
inayopendwa zaidi na wasanii.
Alhamisi ni siku inayotafsiriwa kuwa ni siku ya rangi ya Zambarau.
Zambarau ikilikoza hutambuliwa kama rangi ya kusudio maalum.
NGUVU YA RANGI YA ZAMBARAU
Rangi
hii ni mchanganyiko wa rangi ya bluu na nyekundu kama tulivyosema hapo
awali., Nyekundu ni rangi inayolenga mabadiliko na kutia nguvu na
thamani wakati rangi ya bluu ni rangi inayopooza,kutuliza na ya thamani.
Kwa
mantiki hiyo basi rangi ya zambarau huleta badiliko jipya katika
kuongezeka kwake na kuichochea rangi nyekundi.Kwa sababu hiyo basi rangi
ya zambarau huusishwa namafikiriko na matamanio.
UVAAJI WA RANGI YA ZAMBARAU
Unaweza
kuvaa rangi ya zambarau iwapo unataka kuonyesha ujasiri na kujitia
moyo, sambamba na kuonyesha fikra zako na uwezo wako wa ajabu.
RANGI NYEUPE: INAMAANISHA USAFI NA UHALISIA.
Rangi
nyeupe ni rangi ya uhalisi.Mabibi harusi wengi wanchi mbalimbali
wamekuwa wakivaa rangi nyeupe, kwasababu ni kwamba rangi nyeupe
inamaanisha BIKIRA.
Rangi
nyeupe humaanisha ukarimu.Ingawa katika baadhi ya nchi nyingine nyingi
nguo nyeupe huvaliwa wakati wa mazishi kama desturi zao. Rangi nyeupe ni
rangi ya siku ya Jumatatu kwa wale wanaamini nguvu ya rangi na matukio
ya siku.Vitabu vya kumbukumbu vyeupe huashiria mapenzi ya dhati.
NGUVU YA RANGI NYEUPE.
Tukizungumza
kwa umakini, rangi nyeupe siyo Rangi,bali ni matokeo ya uwepo wa rangi
zote zilizopo ambazo hukamilisha rangi zote za mwanga.Husimama kwa niaba
ya ukamilifu na ujumla.Katika desturi na tamaduni za wengi rangi hii
huwasilisha uwazi na ukweli.Rangi nyeupe imekuwa na kiwango cha
utulivu.Inaweza kuleta ufafanuzi kutokana na nguvu yake kuwa kamili.
Inauwezo
wa kupeleka jambo muhimu mbele katika kila Rangi na hili ndilo
linaloifanya rangi nyeupe kuwa chaguo la wengi katika mwanzo mpya na
maendeleo katika mwelekeo wowote.
UVAAJI WA NYEUPE
Unaweza
kuvaa rangi nyeupe kuonyesha uhalisia na ukamilifu wa kuvutia.Ukiweza
kuzungukwa na nyeupe utajisikia huru na mwenye akili iliyotulia.
RANGI NYEUSI: HUMAANISHA KIFO, DUNIA NA USTAWI.
Rangi
nyeusi ni rangi ambayo haijaweza kueleweka miongoni mwa wengi wetu. Tai
ya Rangi nyeusi ni maarufu kama vazi la kuvaliwa wakati wa chakula
maalum cha usiku na huonekana rasmi na nadhifu.ama wanamke anaweza
kuvalia hivyo akiwa na rangi nyeusi kiasi katika gauni yake.Wakati pia
hata watu wenye nia mbaya au wahalifu huvalia mavazi meusi hasa kofia.
Pia
Rangi nyeusi humaanisha kifo kwa baadhi ya tamaduni na desturi .
Wamarekani mwenyeji hudhani kuwa rangi nyeusi ni nzuri kwasababu
inawakilisha rangi ya Udogo amabo hutoa uhai,.
Rangi hii ni rangi inayosadikika kuvaliwa siku ya Jumamosi.
NGUVU YA RANGI NYEUSI
Rangi
nyeusi na yenyewe tunaweza kusema siyo rangi iwapo tunaongelea kwa
umakini.Ni rangi ambayo haipo miongoni mwa rangi nyingine. Imekuwa ni
kasumba mara nyingi watu wanapozungumzia masuala hasi mar azote
watajuisha rangi nyeusi au nyeupe.Rangi nyeusi na mpinzani wake rangi
nyeupe huwakilisha pande mbili.Rangi nyeusi huakisi rangi zote wakati
nyeupe huushia .Imakuwa ikiitwa kama rangi ya kuficha,kutia hofu au
kupata uzoefu mbaya.Imekuwa ukihusishwa na rangi za kutojulikana au
kutoonekana.
UVAAJI WA RANGI NYEUSI.
Unaweza
kuvaa rangi nyeusi iwapo hutaki kuwa mtu wa kuhisiwa. Pia hutumika
katika uvaaji nguo iwapo unataka kujiwekea utambulisho wako wa
kuwasilisha ujumbe wa ajabu na kwamba unajitawala mwenyewe.Rangi nyeusi
inaweza kusema kuwa “Nitambue lakini usiniingilie.”
RANGI YA NJANO: INAMAANISHA HEKIMA, FURAHA, SHANGWE NA NGUVU YA UFAHAMU.
Mapambo
yaliyosheni rangi za njano humaanisha Uhalisi,Mng’ao na kwamba rangi
ya njano ya jua ni rangi rahisi zaidi kuonekana.Watu ambao mara nyingi
ni vipofu wa rangi huweza kuiona rangi ya njano kwa urahisi zaidi.Rangi
ya njano ni rangi kamili katika ubunifu na nguvu ya ufahamu. Mara zote
tumia karatasi ya njano wakati wa kuandika ujumbe muhimu.
Rangi
ya Njano humaanisha Hekima na Busara.Rangi ya Njano maana yake Furaha
na Shangwe.Watu wenye ufahamu wa hali ya juu hupenda rangi za
njano.Rangi ya njano humaanisha Mapenzi yasiyokifu (KUKINAI).Jumapili
ndiyo siku ya rangi ya Njano.
NGUVU YA RANGI YA NJANO
Kama
ilivyo nguvu ya mwanga wa jua ndivyo hivyo rangi ya njano huleta
utambuzi na umakini.Ukichanganya rangi ya njano na kijani unamaanisha
upokeaji,na hujenga hisia zisizo sahihi.Rangi ya chunjwa na njano
huzidisha hisia za kuwezesha.Njano iliyofifia husaidia kuweka sawa akili
, na pia hufanya akili yako kuwa yenye umakini muda wote.
UVAAJI WA RANGI YA NJANO
Tuvaapo
rangi ya njano tunamaanisha Furaha na kunyanyua hisia. Mara nyingi
unaweza kutumia rangi ya njano ofisini ambayo itakusaidia kuweka sawa
akili, na kuimarisha kumbukumbu na ufanyaji maamuzi.
RANGI YA UDONGO HUMAANISHA: DUNIA, MPANGILIO NA AGANO (AHADI)
Watu
wanaopendelea rangi hii mara nyingi ni watu wanaopendelea mpangilio na
ahadi.Ila maana hasi ya rangi ya njano ni kwamba inawakilisha mtu
kutenda chini ya kiwango au mvuvi.Rangi ya Udongo huwakilisha dunia na
inahusishwa na mahitaji ya maisha.
NGUVU YA RANGI YA UDONGO
Rangi
ya udongo inatokana na mchanganyiko wa rangi nyekundu,bluu na njano,
na pia ni rangi ambayo unaweza kuchanganya na rangi nyingi tu.Rangi hii
inapozidi inafanya muonekano kuwa hafifu.Ingawa pia inaweza kuwa rangi
ya kusawazisha.
Rangi hii inaweza kuleta hisia za umoja na mshikamano, sambamba na kuruhusu kubaki kwenye udongo bila ya kuonekana.
UVAAJI WA RANGI YA UDONGO.
Vaa
nguo za rangi ya udongo iwapo hutaki kuonyesha mwelekeo au hisia na
tabia yako kwa ujumla.Rangi ya udongo ni rangi inayotia maudhi ambayo
hutumika kuficha hali ya ukweli. Kabla ya hapo rangi hii ilitumika
kuvaliwa Na wafanyakazi wa chini (Vibarua).
RANGI YA DHAHABU HUMAANISHA: UTAJIRI, MAFANIKIO NA BUSARA NA HEKIMA.
Haishangazi
kuona kuwa, rangi ya dhababu imekuwa ikitumika Kama ishara ya busara na
hekima sambamba na ishara ya kuwa na Afya njema. Watu wanaopendelea
rangi ya dhahabu Ni watu wenye matumaini makubwa.
Rangi ya dhahabu mara nyingi huusishwa na ishara ya utajiri na mafanikio.
UVAAJI WA RANGI YA DHAHABU
Uvaapo
rangi ya dhahabu kila siku katika maisha yako, hukuongezea nguvu katika
maisha yako binafsi, na pia hukuongezea kujiamini, juhudi na nguvu ya
kutenda kwa uamuzi wako. Uvaaji wa Cheni ya Dhahabu shingoni husaidia
kulinda AFYA.
uchambuzi mzuri na maelezo yameeleweka pia ...asante
ReplyDelete