Kwa wiki nzima
nimekuwa nakusanya mawazo, kutoka kwa wapenzi mbali mbali ambao walikuwa
wananisaidia uchunguzi wangu juu ya namna wanavyoshiriki tendo la ndoa na
kulidhika.
Wengi kati ya
hao kwa kiwango tofauti cha kuanzia mara tatu na kuendelea waliniambia kuwa
hawatosheki na viwango hivyo na kuliacha swali kubaki kuwa wapenzi wakutane
mara ngapi kwa wiki ili watosheke?
Jibu la swali
hili linapatikana baada ya kutambua kitu kimoja muhimu, nacho ni chanzo cha
kutosheka hasa nini? Katika hali ya kawaida kutosheka kupo zaidi akilini na
wala si mwilini, hii ina maana kwamba watu wanaodhani kuupa mwili mahitaji
zaidi kadiri unavyodai ni njia ya kuutosheleza wanajidanganya, kwa sababu tamaa
ya mwili haitoki mwilini bali kwenye akili ya mtu.
Kwa msingi huo
mtu akitaka kutosheka na penzi la mpenzi wake, ni lazima kwanza aitosheleze
akili yake na kile anachopata, zoezi ambalo atalifikia kwa kutathimini uwezo
wake wa kufanya mapenzi na wa mpenzi wake. Wengi kati ya watu wanaodai
hawatosheki kimapenzi ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa
zaidi, bila kuangalia uwezo, nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.
Nikijibu swali
la ni mara ngapi wapenzi wakutane kimwili ili watosheke nitasema hivi:
KUTOSHEKA HAKUNA IDADI, bali ni kwa kila mmoja kulidhika na mwenza wake kutoka ndani
ya akili yake. Kama hapa sikueleweka vizuri katika jibu hilo, maana yangu hasa
ni kwamba kutosheka ni namna mtu mwenyewe anavyoyaendesha mawazo yake.
Ukiyaendesha
mawazo yako kufanya mapenzi mara kwa mara, hutatosheka hata ukipewa kila saa,
kwa sababu fikra zako unazijenga zaidi ya unachopata. Uchunguzi unaonesha kuwa
watu ambao akili zao zimejaa mawazo ya ngono, hawawezi kulala bila kufanya
mapenzi, lakini watu hao hao, ukiwapa matatizo yatakayochukua sehemu kubwa ya
mawazo yao kwa mfano, kuwafunga jela, kuwafukuza kazi, kupata msiba, utashangaa
wanaweza kukata wiki bila kusumbuliwa na tamaa ya ngono.
Hii ina maana
kwamba unavyowaza ndivyo unavyotenda. Kitaalamu kinachofanya mapenzi ni mawazo,
ndiyo maana wapo wanaojichua wenyewe kwa kutumia mawazo yao na kupata raha.
Kila mmoja akijenga heshima juu ya fikra zake na kujali hisia zaidi tutakuwa na
watu wengi wanaofurahia tendo la ndoa bila kujali wanalipata mara ngapi kwa
wiki.
Uchunguzi
wangu umebaini kuwa watu wengi hasa wapenzi wa siku nyingi na wanandoa,
wanafanya mapenzi kwa sababu tu wamepata nafasi ya kuwa pamoja, lakini si kwa
kuheshimu fikra na hisia zao, jambo ambalo husababisha ladha ya mapenzi kuwa ya
asilimia ndogo, ukilinganisha na mahitaji halisi ya mawazo yao.
Upo ushahidi
wa kutosha kwa wanandoa wengi kupata msisimko mdogo wanapokuwa na waume/wake zao
katika tendo la ndoa tofauti na wanapopata wasaa wa kusaliti ndoa kwa hawara zao.
Watu wa aina
hii wasiseme kuwa hawatosheki na tendo la ndoa kwa sababu wanakutana na wapenzi
wao mara chache zaidi, bali wanakutana katika mhemko wa chini usioweza
kulifanya tendo hilo kuwa na raha ya kutosha.
Labda msomaji
wangu utaniuliza, tatizo la kupata msisimko mdogo kwa mtu unayemzoea
linachangiwa na nini? Jibu litakuwa ni MAWAZO ya mtu mwenyewe.
Ukichunguza
utagundua kuwa, wapenzi wengi hasa wazoefu huwa hawapeani nafasi katika mawazo,
kama wanavyotoa nafasi kwa wapenzi wa pembeni,
hili ndilo tatizo linalopunguza msisimko wa kimapenzi na kuondoa hali ya
kutosheka na penzi. Kama mtu anataka mpenzi wake amtosheleze, basi hana budi
kumkuzia mwenza wake hisia kiasi cha kumtamani. Niulize swali, hivi ni mara ngapi wewe unayesema hutosheki na
penzi ulishakaa peke yako ukamvutia taswira
mpenzi wao kabla hajarudi nyumbani kiasi cha kupata msisimko wa kutana
naye kimwili?
Wengi wetu
hatufanyi hivyo, hatuna vitu vinavyotuvutia kwa wake/waume zetu, jambo ambalo
hutufanya tukikutana nao kimwili kwa kutimiza desturi tu na kubaki na kiu zetu
za penzi. Lakini uweli unabaki kuwa wapenzi wakikutana kipindi cha msisimko
mkubwa na kupeana mahaba kwa usahihi hata ikiwa ni mara moja kwa wiki
watatosheka.
Jambo kubwa la
kuzingatia hapa ni kwamba wakati mwingine msisimko huo huwa hauwatokei wapenzi
kwa wakati mmoja, hivyo ni jukumu lao
kushirikiana pindi mmoja anapokuwa katika hali hiyo
No comments:
Post a Comment