Sunday, 10 November 2013

MADHAIFU YANAYODIDIMIZA NDOA/ MAHUSIANO YA KIMAPENZI.






1. Mchanganyiko mkubwa kuhusu maana ya mahusiano, mapenzi na ndoa: Labda kipengele hiki tuanze kwa kueleza kuwa kunaweza kuwepo ndoa, lakini yasiwepo mahusiano wala mapenzi. Inaweza kuonekana kama inachanganya kidogo, lakini ndio ukweli wenyewe. Ndoa ni namna tu ambayo wawili walio kwenye mahusiano wanaamua kuwataarifu rasmi watu wengine kuwa wao wapo rasmi katika mahusiano.

Ndoa ni kiapo mbele ya watu wengine , na ni namna ya kutaka kumuhakikishia mwenza wako kuwa endapo kiapo hicho kitatokea kuvunjika, basi unakubali rasmi kuwajibika kwa mujibu wa taratibu zilizopo za ndoa husika, ikiwemo kukubali kuitwa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kugawanamali, n.k. Na kwa upande wa kiroho, inabeba maana zaidi kuwa unaweka kiapo kwa Mungu wako kuwa utalinda mahusiano yako na huyo unayemchagua. Hivyo basi, ndoa haijengi mahusiano wala mapenzi. Kiuhalisi inabidi kwanza yawepo mahusiano na mapenzi kisha ndio kiapo kifanyike, kwani kinyume cha hivyo nikuwa unakula kiapo 'feki'.
Ndiomaana basi, ni muhimu kwa wapenzi kutambua
kweli kama wanahitajiana, kuwa kwenye mahusiano
na kutafakari kwa uhuru kama kweli wanataka
kuweka kiapo rasmi cha kuwa pamoja. Kutumia ndoa kama kinga ya kuhakikisha mahusiano yako yanadumu ni maamuzi magumu ambayo pengine yanaweza yasilete faida hapo baadae.

2.Mahusiano na ndoa nyingi huyumbishwa na Matarajio yasiyo halisi Kabla hata ya kuingia katika mahusiano na hatimaye ndoa wengi wetu huwa na matarajio binafsi ya kimaisha. Matarajio haya yanajumuisha vile
tunavyotaka sie wenyewe kuwa hapo baadae, pamoja na matarajio ya vile tunavyotaka wenza wetu wawe. Hata hivyo katika hali halisi tunajikuta sisi wenyewe
hatuwezi kujibadilisha au kujiweka kwa usahihi vile
tunavyotamani kuwa (kwa sababu kwa kila tunachojaribu kufanya kuwa bora, tunajikuta bado
tuna madhaifu mawili matatu). Pamoja naukweli
huu, tunajikuta tupo na matarajio ya kuwafanya wenza wetu wawe watu wa aina fulani. Kwa kuwa kiasili binadamu ni kiumbe huru, tunajikuta wenza wetu nao wakiwa 'busy' kutimiza ndoto za vile wanavyotamani kuwa iwe kimavazi, aina yamarafiki, utafutaji wa kazi , kujiendeleza kimasomo, aina ya mali za kununua,hata kufikiria tofauti aina ya maisha wanayotaka muishi.
Matokeo yake ukinzani huu wa matarajio ni mkanganyiko wa mgongano wa mawazo kati ya wawili nyie, na mwanzo wa vita ya chini kwa chini ya nguvu ya maamuzi katika mahusiano yenu.

3. Kuweza kumbadili tabia mwenza wako Mojawapoya jambo ambalo hufanywa na wengi walio katika mahusiano ni kuwa na 'tamaa' yakutaka kumbadili tabia fulani mwenza wake. 


 Hata hivyo 'tamaa' hii ni sehemu yayale tunayoyaita matarajio yasiyo halisi, kwani tabia ya mtu hujengwa na mambo mengi sana, ikijumuisha aina ya makuzi, aina ya mfumo wa imani mtu anaouamini,aina ya marafiki alio nao, uwezo wake wa kujiamini katika kubadili tabia kwaniwengine wameshakata tamaa kuwa hawawezi kukata tamaa, na zaidi sana, mabadilikoya tabia huhitaji mfumo endelevu na wenye kusoma vema asili ya tabia ili kuweza kuirekebisha. Hata hivyo wengi wetu kwenye mahusiano, hutegemea 'mapenzi'au vitisho tuu kama
vile'nitakuacha mie ', kama sababu yakumfanya mtu
abadilike kitabia.Udhaifu wetu katika kutambua asili
ya tabia yamtu husika na mbinu za kisayansi za kubadili tabia hufanya zoezi la kubadilishana tabia
kuwa gumu na pengine lisilowezakana.

4. Kuvumilia ndio kuonyesha upendo na ndio kudumisha mahusiano Hii ni aina nyingine ya matarajio ambayo sio halisi kwani kiukweli kila mtu analo jukumu la kufanya bidii kuwa mtu mwema, hivyo hauhitaji kubeba 'uzembe' wa mwingine kwa kisingizio tu cha kuwa
unaonyesha upendo hususani pale ambapo ni kwa
uzembe tu au kutokujali kwake mwenza husika amefanya jambo fulani. Kwa jinsi kasumba hii ilivyo enea sio ajabu kukuta mtu akifanya mambo mabaya kwa mwenza wake kwa makusudi ili tu eti apime kama kweli mwenza wake ni mvumilivu. Kumbuka hapa hatumaanishi kuwa kusamehe ni kosa. Hapana, kusameheana ni muhimu, lakinisio kwamba ni muhimu tu katika mapenzi. Kusameheana ni jambo la asili, na tunapaswa kusameheana kwa mambo mengi nje hata ya mahusiano. Tunachosemani kuwa kuna kasumba ya baadhi yetu kuona kuwa wanayo 'haki' ya msingi ya
kukosea eti tu kwa kuwa tu mwenza wake analazimika kusamehe ili kuonyesha kweli anao upendo wa dhati.

Amini usiamini, kasumba hii ya kutarajia aina ya pekee ya kusamehewa na kuvumiliwa kwa kisingizio tu cha kuwa upo kwenye mapenzi na mwenza wako, hurudisha nyuma maendeleo ya mahusiano yenu kwani mwenzi wako nae ni binadamu na kumbuka anayo matarajio mengine ya maisha,isitoshe na yeye anahitaji upendo na kujaliwa na wewe, hivyo kutarajia kwako kusamehewa na kuvumiliwa kuna mnyima haki mwenza wako. Hatimaye kutegema kwako kusamehewa kila wakati, kunamfanya mwenza wako atilie mashaka upendo wako kwake. 


5. Uaminifu = Upendo= Kudumu kwa mahusiano Pamoja na ukweli kuwa mwenza wako anatarajia
utakuwa muanifu kwake, elewa kuwa kuwa mwaminifu pekee katika mahusiano yako sio tiketi ya kudumu kwa mahusiano yenu kwa kuwa watu wanaingia kwenye mahusiano sio tu kwa kuwa wanataka kuwa na mtu mmoja muaminifu bali wana mahitaji mengine wanayohitaji. 


Zungumzana mwenza wako, fanya utafiti wako binafsi kuhusu mpenzi wako ujue mambo mengine anayohitaji toka kwako. Pia msikilize anapokutaka urekebishe mambo kadhaa au ufanye mambo fulani. Inapendeza pale unapomfanyia mtu
mambo yanayompendezesha kwa kuwa hivyo ndivyo
anavyotaka, sio kwakuwa tu wewe unadhani kufanya hivyo kutampendezesha mhusika.

No comments:

Post a Comment