Mapenzi yanataka elimu, lakini si wote wanaojielimisha namna ya kuwafanya wapenzi wao wajione kuwa ni sawa
alama na hivyo kuwafanya mapenzi yao kudumu kwa muda mrefu.
Wanaume wa siku hizi wamekuwa hawafahamu ni vitu gani ambavyo wanawake
wanapenda kuvipata kutoka kwao.
Kushindwa kuwa na elimu hii, wanaume wengi wamejikuta
wakitumia ukali kuwatawala wake zao, jambo ambalo limekuwa likizidisha
migogoro ya kimapenzi na hatimaye wapenzi huachana. Yafuatayo ni mambo
muhimu ambayo wanawake hupenda watendewe na wapenzi wao.
KUTATULIWA MATATIZO
Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi
watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa
mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha,
kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya
jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa
za kuteka penzi la mwanamke.
KUBEMBELEZWA
Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni,
wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono
wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi
mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi
hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.
KUWA NAMBA MOJA
Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na
kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete
ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi
huhitaji ni kuwa namba moja au kupendwa.
Wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na
mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla.
Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au
kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya.
KURIDHISHWA KWENYE TENDO
Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya
mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa
utayumbisha penzi lako. Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa
anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo. Utundu unahitajika ili
kumkata kiu mpenzi wako.
MAZUNGUMZO
Wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, huku
wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, hii ikiwa na
maana kuwa wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine.
Kwa msingi huo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu
ya kueleza mawazo yao. Kama una mpenzi wako mpe uhuru wa kuzungumza na
kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali.
No comments:
Post a Comment