Hata
kama utapingana na mimi, lakini ukweli utabaki pale pale; Kila jinsia
inahitaji sana kuungana na jinsia nyingine katika tendo muhimu na la
kihistoria katika maisha liitwalo ndoa! Yes, huu ni ukweli ambao upo.
wazi na utaendelea kusimama kama ulivyo.
Jinsia zote zina umuhimu na jambo hili muhimu, lakini kuna tofauti kidogo, kwamba mwanamke
anasubiri
kufuatwa na mwanaume, wakati mwanaume anaamua kumfuata mwanamke
anayemtaka na kwa wakati wake. Kuna kitu nataka kuweka sawa hapa,
kwamba wanaume
ndiyo
huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa
wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume
husika.
Wanawake
wa ‘mjini’ huwa hawakubaliani na hili, kutokana na huu utandawazi
unaohubiriwa siku hizi ikiwa ni pamoja na kampeni za usawa zinazotetewa
na Wanaharakati Wanawake. Akina dada nao huchangamkia kueleza hisia
zao kwa wanaume. Nadhani si jambo baya, ingawa linaweza kupokelewa kwa
hisia tofauti na kila mwanaume.
Tuyaache
hayo, hoja kubwa ya msingi hapa ni jinsi gani mwanamke anaweza kuolewa
haraka na mpenzi wake. Ikumbukwe kwamba, hapa nazungumza na wanawake
ambao tayari wapo katika uhusiano, lakini wenzi wao hawana habari
kabisa na mambo ya ndoa.
Katika
matoleo yaliyopita, niliwahi kuzungumza kuhusu namna gani mwanamke
anaweza kuwashawishi wanaume wakataka kuingia katika uhusiano naye. Leo
nazungumzia juu ya wewe ambaye upo katika uhusiano ambao haueleweki,
lakini ndoa unaitaka. Unajua cha kufanya? Fuatana nami.
EPUKA MAKUNDI HATARI
Mwanaume
anapenda kuwa na mke mwenye staha, ambaye hana tabia za hovyo. Kuwa na
makundi ya ‘mashangingi’ ni alama ya kwanza kabisa kuwa unapenda au
tayari una tabia za kishangingi. Wanaume wengi hawapendi kabisa
wanawake wenye tabia za hovyo, wenye kampani ambazo si nzuri.
Lakini
yawezekana, jamaa alishakuambia juu ya kilio chake hiki, lakini wewe
umekuwa kama umeweka pamba masikioni mwako, hili ni tatizo. Linda
heshima yako, kaa mbali na makundi hatari, ili umfanye jamaa akuone
wewe ni mwanamke thabiti ambaye huigi, hushabikii na wala huna tabia
mbaya. Utaonesha hili kwa kukaa mbali na makundi ya wanawake hatari!
Umenipata?
ZINGATIA MAVAZI YAKO
Kila
mtu anamjua mtu wake alivyo, mwanamke hata wewe unamjua mpenzi wako
alivyo. Sina shaka unafahamu anapenda nini na nini anachukia. Unajua
kabisa, nina uhakika na hilo. Lakini pamoja na kwamba jamaa anaweza
kuwa na vitu ambavyo vinamvutia zaidi, hata wewe kama mtoto wa kike,
una mapendekezo yako au vitu ambavyo unapenda zaidi kuvifanya!
Huzuiwi,
lakini swali la msingi, mwenzi wako anapenda? Kama wewe unapenda sana
skin jeans na top inayoacha kitovu nje, yeye hapendi kwa sababu ana nia
ya kukufanya mke hapo baadaye. Sasa utakuwa mke gani ambaye hata Salim
anaona sehemu zako za faragha hadharani?
Ukiachana
na chaguo la mwenzi wako, lakini lazima wewe mwenyewe kama mwanamke wa
mtu, ujitambue! Jisitiri vyema. Kwani kuna urembo gani wa kuvaa nguo
inayoonesha mwili wako ulivyo? Kuna burudani gani kuacha nyeti zako
wazi? Unataka nani akuone ulivyo? Mke hana sifa hiyo dada yangu, sasa
ili uweze kuwa na sifa hii muhimu, lazima uzingatie sana mavazi yako.
JIPE MOYO
Hili
nilishawahi kulizungumza sana katika mada zilizopita, baadhi ya
wanawake wamekuwa wakikatishwa tamaa na rafiki zao au watu wengine
wanaowazunguka, eti hawana hadhi ya kuolewa au watahangaika sana lakini
hawatapata mume, kisa eti HAVUTII!
Mwingine
anajinyima mwenyewe nafasi akisema; “Mimi nina balaa, sina bahati ya
kuolewa, ndiyo maana wadogo zangu wote wameolewa nimebaki mimi.”
Huu ni uvivu wa kuwaza. Lakini dada yangu, habari iliyo njema kwako ni kwamba, ndoa unaitengeneza wewe mwenyewe.
Unaitengeneza
kwa misingi ya kwanza, kujipa moyo mwenyewe kwamba wewe ni mzuri na
una sifa na haki za kuolewa kama wanawake wengine. Jipe moyo mwenyewe,
huna nuksi wala balaa, wewe ni mzuri na una sifa za kuwa mke hapo
baadaye.
Iko
hivi, ukianza kujishusha mwenyewe, ni dhahiri kwamba hata mavazi yako
hayatakuwa mazuri, uso wako hautakuwa na tabasamu na wala hutakuwa na
matumani moyoni, hapo sasa ni mwanzo wa kuzorota afya yako. Utapata
mchumba kweli? Utasubiri sana kwa mtindo huo.
ACHA PAPARA
Haizuiwi
kuuliza kuhusu mustakabali wa uchumba wenu, lakini ni vizuri basi kuwa
na kiasi. Kuuliza kila wakati au kuwa mtu wa kulaumu, hakutakusaidia
kumfanya jamaa achukue maamuzi ya haraka ya kukuoa na badala yake
yanaweza kumpa picha tofauti.
Ni
rahisi kuwaza kwamba, unachohitaji kwake ni ndoa na baada ya hapo
hutakuwa na staha tena. Kuwa mjanja, achana na papara. Usilogwe
ukamfanyia jambo zuri mpenzi wako, halafu ndiyo umuulize; “Sasa honey,
mbona hata huzungumzii ndoa yetu? Hivi utanioa kweli? Eeeh baby?
Niambie basi mpenzi wangu.
No comments:
Post a Comment