Sunday, 18 May 2014

USIPOZIDISHA MAPENZI KWA MWENZA WAKO HIKI NDICHO ATAKACHOKUUMIZA NACHO!!

Wachumba
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Gothenberg, Uswizi, wanaume wengi huwapuuza wachumba wao wanapoburudishana faraghani.
 
Utafiti huo unasema wanaume huongozwa na ubinafsi wanaposhiriki tendo la ndoa na kusahau kwamba wachumba wao wana hisia.
 
Kulingana na utafiti huo wa 2009, ingawa wanaume wengi wanaelewa umuhimu wa kuwandaa wachumba wao kabla ya kuanza burudani,hawajali yanayowapata wenzao wasipopata shibe la ngoma.
 
“Suala la wanaume kutowaridhisha wapenzi wao linatokana na kukosa kuwaandaa vyema. Mwili wao husisimka haraka wanapopandwa na hamasa ya kushiriki tendo la ndoa.Wanasahau kwamba mwili wa mwanamke ni tofauti,” yasema sehemu ya utafiti huo.
 
Watalaamu wa masuala ya mapenzi wanasema mwanaume mwenye tabia hii huwa hawezi kumfikisha mwanamke kileleni.
Wanasema ni wazi kwamba mwanamke asipoandaliwa vyema, hawezi kufurahia burudani.
 
“Tabia hii ya wanaume imefanya watemwe na wachumba wao. Wanawake wanataka mwanaume anayetambua na kuelewa hisia zao, sio wa kuwatumia kama chombo cha kutimiza haja zake za kimwili bila kujali wanavyohisi,” asema mwanasaikolojia Ronald Jameson.
Anasema mwanaume anayeanza kufanya mapenzi kwa pupa, hawezi kujizuia kufunga bao baada ya sekunde chache na kumuacha mpenzi wake akitamani burudani.
 
“Huwa vigumu kwa wanaume wa aina hii kurudia ngoma jambo ambalo wanawake wengi huchukia” asema.
 
Wataalamu wengi wa mapenzi wanabainisha kwamba wanaume wanaotumia muda mwingi kuwaandaa wachumba wao kwa burudani, huweza kujizuia kufunga bao mapema na hivyo hufanikiwa kumfikisha mwanamke kileleni zaidi ya mara moja.
 
Kujali hisia
“Uhusiano wa aina hii ambapo wanaume wanajali hisia za wapenzi wao hudumu kwa muda mrefu, furaha utawala na mapenzi hunoga huku kila mmoja akimwaza mwenzake kila wakati na kutamani burudani zaidi,” aeleza Jameson.
 
Anasema mbinu na muda wa kumwandaa mwanamke hutegemea mtu binafsi.
 
“Kuna wanawake wanaosisimka wanapoguswa sehemu tofauti za mwili na wengine hupandwa na hamu ya kufanya mapenzi wanapobusiwa. Wengine wanaingiwa na hamasa kwa kumtizama mwanaume anayewavutia” asema.
 
Wataalamu wanawakosoa baadhi ya wanawake kwa kuchangia misukosuko ya mapenzi hasa kukosa shibe la burudani kwa kutowaongoza wanaume wao kwa maneno ama kwa kuweka mikono eneo wanalotaka washikwe ili kuamsha hisia zao za mapenzi.
 
“Ni rahisi kwa mwanamke kufanya mchumba wake ashindwe kusakata ngoma ipasavyo kwa kutoshiriki kikamilifu katika mechi kitandani” asema.
 
Wataalamu wanasema baadhi ya wanawake huwa hawana ujasiri wa kumwongoza mwanaume kumtomasa sehemu inayoamsha hisia zake za kufanya mapenzi. Jambo hili, asema Jameson, huwanyima raha ya burudani na kusambaratisha penzi. Hata hivyo ili kumwandaa mwanamke wa aina hii, watalaamu wanasema mwanaume anapaswa kutumia ujuzi wa hali ya juu ili kuamsha ashiki zake.
 
Ili zoezi la kusakata ngoma lifanikiwe na kufanya uhusiano wa mapenzi huwe thabiti, mwanamke anatakiwa kuonyesha ushirikiano kwa kutoa miguno na minongono ya kumchanganya mwanaume.
Kulingana na utafiti wa chuo kikuu cha Gothenberg, wanawake hawaridhishwi na tabia ya wapenzi wao kupuuza umuhimu wa kuwaandaa kabla ya kufanya mapenzi.
 
Watafiti wanasema wanawake wanachukia wanaume wenye pupa ya kufanya mapenzi. Na huenda afueni isipatikane kuhusu hali hii huku wanaume wakiwalaumu wanawake kwa kukosa uwazi katika swala la mapenzi kwa kutowaeleza wanaume kwamba hawako tayari.
 
Kukubaliana na utafiti
Wanawake wengi nchini walikubaliana na utafiti huo wakisema unaeleza jinsi mambo yalivyo. Wanafananisha hisia za mapenzi za mwanaume na jiko linalotumia mafuta ya taa linalowaka kwa haraka kisha kuzimika, na mwanamke na jiko la makaa linalochukua muda kuwaka na halizimiki kwa haraka.
 
“Mwanamke ni sawa na jiko la makaa linalohitaji bidii kulichochea liwake, na likishawaka ni kazi ngumu kweli kulizima,” asema Bi Ruth Wanjiku.
 
Mwanadada huyu anakiri ushirikiano wa hali ya juu ni muhimu kufanikisha burudani kitandani .
 
“Ni kweli wanaume wana haraka ya kufanya mapenzi na humaliza shughuli hata kabla ya mwanamke kuanza kuwaka. Hata hivyo baadhi ya wanawake wanachangia kwa kutoshiriki kikamilifu wanaporushana roho,” asema Bi Wanjiku.
 
Anakubaliana na watafiti waliofichua kwamba wanawake wanachangia kufanya wanaume wapungukiwe na nguvu za kufanya mapenzi kwa kutohusika ipasavyo.
 
“Ni muhimu kwa wana ndoa au wapenzi kufahamiana vyema ili waweze kusisimuana,” aeleza Bi Mary Kituyi mkazi wa jiji la Nairobi. Anasema wapo wanaume wasiowapa wachumba wao nafasi ya kuonyesha ustadi wao wa kurushana roho.
 
“Kuna wanaume wanaoamini kwamba mwanamke hafai kumfundisha mambo ya mapenzi. Ukijaribu kumwelekeza unakotaka uguswe au mbinu unayofurahia anaanza ugomvi,” anasema na kuongeza kwamba uhusiano wa aina hii hauwezi kudumu.
 
Kulingana na mwanasaikolojia Peter Obonyo wachumba wanaokabiliwa na tatizo hili wanaweza kulisuluhisha bila ya kuachana.
 
“ Dawa la tatizo hili sio kumwacha mchumba wako, mbali ni kumzungumzia kwa lugha ya mapenzi na sio kwa ukali,” asema.
Anashauri wanaokabiliwa na tatizo hili wasome vitabu au majarida yanayotoa elimu juu ya kufanya mapenzi na wataalamu wa mapenzi kwa ushauri.
“ Wakishapata elimu ya kutosha na kuizingatia, watajitayarisha kisaikolojia na utashangaa mwanamke anafika kileleni kabla ya mwanaume. Hakuna miujiza hapa, ni mambo ya kisaikolojia tu,” asema.
Kulingana na mwanasaikolojia huyu wanaowaacha wachumba wao kusaka shibe la mapenzi, hukabiliwa na hatari nyingi.
 
“Wanaweza kugeuka kuwa wahamaji wa mapenzi kwa kubadilisha wachumba kila mara. Pia kuna hatari ya kuathirika kisaikolojia na kukosa utulivu wa kihisia,” asema.
 
Maandalizi ya mapema
Kulingana na wataalamu mawasiliano ni muhimu kati ya wapenzi ili kila mmoja aweze kumwandaa mwenzake vyema na kwa upendo kabla ya kushiriki tendo la ndoa.
 
“Maandalizi huwa kwa njia nyingi.Mazungumzo yenu, usafi wa nguo, mwili na chumba murua cha kuandalia burudani ni muhimu,” asema na kuongeza kwamba mwanaume anafaa kuonyesha utulivu na kujali hisia za mpenzi wake.”
 
Pia mwanamke hafai kuona aibu kumuongoza kipenzi chake ili wafurahi pamoja.
 
Kulingana na Bi Wanjiru mwanamme mwenye upendo hufurahi sana ikiwa mpenzi wake atafunua hisia zake. Anasema kwa kawaida si rahisi wanawake kuelezea hisia zao kwa maneno na wanaume wanafaa kufahamu ishara za wachumba wao wakiwa tayari kuteremka katika bahari ya mapenzi.

No comments:

Post a Comment