Tuesday, 9 July 2013

BONDIA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU......ALIKUWA AKIAMULIA UGOMVI KABLA YA KISANGA KUMGEUKIA


BONDIA  maarufu Ramadhani Idd ‘Mashudu’ ameuawa kwa kuchomwa visu mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lililowaacha midomo wazi wakazi wa Mabibo Loyola, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam lilitokea saa sita usiku Julai 4, mwaka huu.

Imedaiwa kuwa, marehemu aliwakuta Jack Mchaki na mtu mwingine wakigombana, alipowaamulia wakamgeuzia kibao na kumchoma visu.

Waandishi wetu walifika eneo la tukio na kukutana na mashuhuda waliozungumza kwa sharti la kutoandika majina yao , mmoja alidai marehemu alikuwa anaangalia kanda za filamu katika banda moja maeneo hayo ghafla alifika Jack aliyelewa na kuanza kufanya fujo.

Shuhuda huyo alisema: “Kitendo kile hakikumfurahisha  kijana mwingine, hivyo wakaanza kupigana ndipo Mashudu akawaamua.”

Aliongeza kuwa, baada ya kuamuliwa mtuhumiwa alikwenda nyumbani kwake akabadili nguo kisha akarudi tena na kumkuta Mashudu akiendelea kuangalia filamu, akaanzisha ugomvi tena na bondia huyo kumbe kiunoni alikuwa na kisu.


Walianza kupigana na baada ya kuona anazidiwa nguvu alichomoa kisu akamchoma Mashudu tumboni, kichwani na kumsababishia kuvuja damu nyingi kisha akatoweka.


Alisema walitafuta usafiri na kumpeleka majeruhi Hospitali ya Palestina Sinza, walipofika madaktari wakawaambia tatizo lake lilikuwa kubwa hivyo apelekwe Hospitali ya Mwananyamala.

“Tulipofika Mwananyamala alipopimwa na daktari Mashudu akathibitika kuwa amekata roho kutokana na kuvuja damu nyingi,” alisema shuhuda huyo.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

No comments:

Post a Comment