Matatizo yanayochangia watu kuachana yako mengi, ambayo mtu unaweza
kujaza vitabu kuyaelezea, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi
huachana kutokana na udhaifu wa sababu zilizowasababisha kupendana. Kwa
mfano wapenzi ambao wakati wa kupendana kwao walitamaniana kwa maumbo,
sura, mvuto wa kingono na pesa huwa katika hatari ya kuachana baada ya
vitu vilivyowasukuma kupendana kupoteza mvuto.
Hakuna asiyefahamu
kuwa watu hubadilika tabia, umbo, sura, hufirisika na hata kutovutia
tena! Hivyo mtu anapopenda kwa sababu hizo, ukomo wake huwa ni baada ya
alichopenda kuondoka. Ukipenda kwa tamaa ya ngono ukishashibishwa nayo
hutakuwa na sababu ya kumpenda mpenzi wako, matokeo yake utamwacha.
Ukiwa
umeamua kumpenda dada fulani kwa sababu anavutia, kumbuka kuwa anaweza
kupata ajali akapoteza mvuto au akazeeka. Je umeshajiuliza swali
itakuwaje kama mpenzi wako atapata
makovu, utafanyaje baada ya mvuto wake wa usichana kuisha, nini
kitafuata baada huyo mwanaume unayemsifia kwa tendo la ndoa atakapofikia
ukomo wa kukutosheleza? Nadhani ni kuachana.
Sababu
nyingine inayochangia wapenzi kuachana ni kutojali changuo sahihi
kulingana na jinsi mtu mwenyewe alivyo,
Mimi niliwahi kusoma katika
Biblia Mungu akiweka wazi namna alivyozingatia kumuumbia mke Adamu kwa
kusema, alimuumba mtu wa kufanana naye. Hivyo ni busara kupata mpenzi
wa kufanana na wewe kwa tabia na mambo mengine ya msingi, bila hivyo
mapenzi hayawezi kudumu.
Kwa mfano kama
wewe ni mtu wa imani kali, inakuwaje unakwenda kupendana na mpagani,
huoni hicho kitakuwa kikwazo cha penzi lenu? Kwa msingi huo, lazima
kupendana kuambatane na kufanana elimu, mtazamo na hata tamaduni, hii
itasaidia kuondoa vikwazo vya mapenzi kuvunjika.
Lakini
jambo jingine linalowafanya wapenzi wengi kuachana ni kutojali au
kutofahamu kanuni za kutunza penzi. Kuna watu wanaweza kuchaguana kwa
kuzingatia maelekezo yote, lakini wakajikuta wanaachana kwa kutojua
namna ya kukuza na kudumisha upendo wao.
Nasema hivyo kwa
sababu, kumpata mpenzi ni jambo jingine na kumtunza ni hatua nyingine
ambayo ni ya msingi. Inawezekana kabisa ukampata wa kufanana naye,
lakini ukajikuta unashindwa kudumu naye kwa sababu ya kumuudhi mara kwa
mara tena kwa kusudi, kumnyanyasa, kusikiliza umbea, wivu, kutomjali na
kumpuuza.
Kinachosikitisha sana
katika mapenzi ni kuona watu wanawapata wapenzi wa kweli, badala ya
kufurahika nao wanawachezea kwa kufanya vurugu na kuwa waanzilishi wa
usaliti na ujeuri. Ushauri wangu ni kuwa, ukipata wa kukupenda
usimchezee, mtunze na umuonyeshe kweli kuwa wewe ni wa kufanana naye.
Mwisho,
mapenzi lazima yakose sababu, ukiulizwa unampendea nini mpenzi wako?
Jibu liwe sijui, kwani ukitaja sababu yoyote unakuwa katika hatari ya
kuachana kwa vile kila sababu ina mwisho wake. Penzi ni lidhiko la moyo
lisilokuwa na kwa nini. Ukisema nampenda kwa sababu ananijali,
asipokujali, ukisema ni mzuri akiwa mbaya, ana pesa akiishiwa, mtundu
uwanjani akichoka? Bila shaka penzi nalo litachoka!
No comments:
Post a Comment