Wapenzi wengi hasa wale ambao uhusiano wao ni mchanga hupenda sana
kufanya mapenzi kila wanapokutana au wanapohisi wamehemkwa na miili
yako. Watu wa aina hii ni wale ambao wanatoka katika kundi la mapenzi ya
kisinema niliyoeleza katika kitabu cha TITANIC No1.
Katika
hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja
suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara
kwa watu wanaoendekeza sana
ngono. Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku
wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu
anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’
kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo
kwa sababu amelipa mahari. Hilo
linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi
unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za
kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.
Pamoja na tatizo hilo,
yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo
la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe
watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila
tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu
miili imetaka kufurahika. Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa
kina.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO
Watu
wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa
wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza
wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara. Sababu hizo zinaweza
kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata
anapomuona akiwa mtupu.
Aidha
kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na
kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu
moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya
mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye
na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA
Tabia
ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini
na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo
la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa
kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa
wakati gani?
Watu
wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao
kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake. Hawa
ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au
kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa
zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi. Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara
kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka
siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO
Raha ya tendo hutegemea sana
hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi,
hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza
msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza
tamaa yako. Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili. Kama
tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi,
hivyo kuufanya mwili uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya
mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.
Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.
KUPATA MAGONJWA
Kama
tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa
na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia
magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na
msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na
kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko
wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza
kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
Baada
ya kungalia madhara hayo machache ni vema kwa wapenzi kupunguza kiwango
cha kufanya mapenzi ili kuifanya miili iwe na uvumilivu unaoweza
kumsaidia mtu kukaa kwa muda mrefu bila kumsaliti mpenzi wake hata kama atakuwa amesafiri mbali naye kimasomo, kikazi au kibiashara.
No comments:
Post a Comment