Mpenzi msomaji wangu, ni
wakati mwingine ambao tunakutana katika uwanja huu wa maisha na mapenzi, kwa
lengo la kujifunza namna ya kuwa wapenzi bora na kuepukana na tatizo la
kuachana ambako kumekuwa fasheni siku hizi.
Vijana wengi ambao wanapendana
leo mapenzi yao
hayadumu kiasi cha kubatishwa jina la utamu wa bazoka. Lakini yote hii
inatokana na ukweli kwamba elimu ya mapenzi ambayo ni muhimu kwa binadamu
haitolewi ipasavyo.
Ipo zana potofu kwamba
kumfundisha motto mapenzi ni kumharibu, jambo ambalo si kweli bali inategemea
mtoto huyo anafundishwa nini na kwa wakati gani. Lakini cha kushangaza zaidi
hata watu wazima ambao ni wadau wa mapenzi hawayajui, matokeo yake wanajiingiza
kwenye uhusiano wakiwa bumbumbu na hivyo kuteshwa na changamoto za mepenzi.
Leo tutajifunza kwa undani
sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa
mioyo na utu wetu. Sifa hizo hizi zifuatazo.
KWANZA: Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini
unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.
PILI: Ni yule atakayejua
wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .
TATU: Ni yule atayekuwa
tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri .
NNE: Atakuwa na wewe wakati
wa shida na raha. Hatakuacha mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na
raha.
TANO: Mpenzi wa kweli
atakuheshimu na hatopenda kuwa nyuma na kukuacha bila msaada .
SITA: Atakupenda kwa moyo
wake wote na wala si kwa ajili ya
shinikizo fulani (pesa au mali)
SABA: Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine
NANE: Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila
kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.
TISA: Mpenzi wa kweli ni yule
anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama
atalazimika kufanya maamuzi magumu .
KUMI: Atakuwa tayari
kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.
No comments:
Post a Comment