Mwigizaji mwenye muonekano wa kipekee katika tasnia ya filamu
Bongo Lumole Matovolwa ‘Biggie’ anasema kuwa alikosa kwenda kuigiza
filamu Ulaya kwa sababu ya kwenda kurekodi filamu
mbali na ukosefu wa
ratiba nzuri katika filamu za Tanzania umfanya kuchelewa alipofanya
usaili kwa ajili kwenda kushiriki katika filamu ya Afrika iliyotakiwa
kuanza kurekodiwa nchini Ujerumani alisafiri nje ya mjini na
kutopatikana katika simu.
“Iliniuma sana baada ya kurudi na kukuta ujumbe ambao nilikuwa
nimepewa maelekezo kwa ajili ya kumuona mhusika kusafiri na kuungana na
wasanii wa nchi mbalimbali kwa ajili ya utengenezaji wa filamu na mimi
muonekano wangu wa kipekee uliwavutia sana wazungu,”anasema.
Biggie anasema pamoja na kukosa nafasi hiyo kwa kuchelewa
kuwasiliana na wahusika alijisikia vibaya lakini kwa sababu lengo lake
ni kuwa msanii wa kipekee katika tasnia ya filamu kwa ukanda wa Afrika
Mashariki na kati amekuwa makini sana anapopata nafasi kwa ajili ya
kuigiza, ndio akiwa kama mhusika mkuu katika filamu ya Mdundiko ameweza
kufanya makubwa na filamu hiyo kuibuka na ushindi nje ya nchi.
Filamu ya Mdundiko ilishinda tuzo ya hadithi bora ya asili
katika tamasha kubwa la Silicon Valley African Film Festival (SVAFF
2013) sinema ya Mdundiko ilinyakua tuzo ya (Achievement Narrative in
Feature Film) iliyotolewa katika jumba la sinema la San Antonio Circle
Mountain View, katika Chuo cha Muziki na Sanaa California, Marekani.
No comments:
Post a Comment