Picha ikimwonyesha mtoto Zakaria (1) na jeraha lake lililotokana na kung’atwa na baba yake.
Inawezekana hakuamini hivyo kwa kuwa mume wake Matata Makali (siyo jina halisi), ambaye alionekana mwenye upendo na kujali, pengine ni kwa sababu ya mapenzi mapya ya binti mdogo.
Wakati alipoolewa kuwa mke wa pili kwa mahari ya ng’ombe wanane, Katarina Mturi (22) alisindikizwa kwa ngoma na tamaduni za Kabila la Kikurya, wala hakuamini kama kuna siku ataichukia ndoa hiyo.
Inawezekana hakuamini hivyo kwa kuwa mume wake
Matata Makali (siyo jina halisi), ambaye alionekana mwenye upendo na
kujali, pengine ni kwa sababu ya mapenzi mapya ya binti mdogo.
Katarina alikuwa ameolewa mara ya pili akitoka kwa
mume wake wa kwanza aliyedai hakuwa na hata chembe ya upendo ndipo kwa
kushauriana, familia yake ilimrudishia mahari mwanaume huyo na ndoa
kuvunjika.
Mwanamke huyo anasema kuwa alikaa nyumbani kwao kwa muda, ndipo akajitokeza Matata(45), akiamini kuwa sasa amepata mume mwema.
Hata hivyo, hali ilikuwa kinyume, kwani leo
Katarina ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Chinato, kijijini Bisarara,
Kata ya Sedeco katika Wilaya ya Serengeti iliyopo Mkoa wa Mara, amekuwa
miongoni mwa wanawake wanaosimulia ukatili wa kijinsia katika ndoa.
Kutokana na yaliyomkuta, anaona kuwa ndoa siyo tena hitaji lake muhimu
maishani.
Kwa nini?
Pamoja na mateso, kipigo alichokuwa akipata,
alijitahidi kuvumilia familia yake ikimtia moyo na kumweleza kuwa ndoa
ndivyo zilivyo.
Lakini Katarina anasema hatosahau tukio la saa
2:30 usiku, Januari 8 mwaka huu, ambapo mumewe huyo mpya alimfanyia
ukatili bila kuwa na chembe ya huruma.
Katarina anaeleza kwamba hofu yake sasa ni ukatili kumwachia ulemavu.
“Katika hali ambayo mpaka leo sijaielewa, nilikuwa
ndani na wanangu wawili, mkubwa na huyu mdogo mume wangu aliingia ndani
akaniamuru niswage ng’ombe usiku huo kwenda ndani ya Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti kwa malisho. Nilikakataa, kwa sababu ilikuwa ni usiku.
Nilimweleza kuwa kisheria haikubaliki kuchungia mifugo ndani ya Hifadhi
ya Taifa, tena kuna wanyama wakali na mimi ni mwanamke nitafanyaje?,”
anasimulia.
Katarina anaongeza akionyesha maeneo aliyoumizwa: “Maneno hayo yakamkasirisha na kilichotokea ndiyo kama unavyoona.”
Anasema kuwa mume wake alichukua fimbo na kuanza kumpiga mithili
ya mbwa mwizi, bila kuchagua sehemu ya kupiga na kumuumiza maeneo
mbalimbali ya mwili ikiwamo mguu, ambao sasa uko hatarini kuoza.
“Akanipiga mpaka mwenyewe akachoka; sikuwa na
uwezo wa kukimbia kwani damu zilinitoka mno na mtoto alikuwa akilia
baada ya kuona ninavyopigwa. Lakini mwanaume huyo hakuwa hata na chembe
ya huruma. Nikitafakari kosa langu sijui, nadhani alikuwa amepanga kwa
muda mrefu kutekeleza lengo hilo,”anaeleza.
Baba amalizia hasira kwa mtoto
Katarina anasimulia kuwa baada ya kipigo hicho
alichopata yeye, Matata alimrukia mtoto wake na kumng’ata meno mgongoni,
akidai alimpandisha hasira baada ya kulia alipomwona mama yake (yeye
Katarina) anapigwa.
“Bila chembe ya huruma aliamua kumrukia mtoto wa
mwaka mmoja na kumng’ata mgongoni mpaka akamtoa nyama. Licha ya mtoto
kulia kutokana na maumivu makali aliyopata, Matata hakujali, hata mimi
kudhani kuwa mwisho wetu na mwanangu ndiyo umefika,”anasimulia Katarina.
Agoma kuwapeleka hospitali
Licha ya majeraha waliyopata usiku huo wa Januari
8, siku iliyofuata ya Januari 9 Matata aliamka na kuendelea na shughuli
zake, bila kujali, wala kuwa na dalili za kuwapeleka hospitali mkewe na
mwanawe ingawa aliona kuwa mkewe hakuweza kutembea kutokana na jeraha na
maumivu aliyokuwa nayo.
Mama abeba jukumu
Meremo Mturi (43), mama mzazi wa Katarina anasema
kuwa akiwa nyumbani kwake katika shughuli zake za kawaida, ghafla
alimwona binti yake (Katarina) na mjukuu wake wakisindikwa hadi nyumbani
kwake hapo.
“Nilipowaona nilistuka nikajua kuna jambo lisilo
la kawaida wametendewa, ndipo Katarina akanisimulia nami nikashuhudia
hali halisi, niliogopa sana,”anasema.
No comments:
Post a Comment