Thursday, 30 January 2014

LAANA HII:MESENJA wa Mkuu wa Wilaya KISARAWE matatani kwa Shutuma za kumbaka Mtoto wa darasa la Kwanza.

mtoto1
DUNIA inaelekea ukingoni. Mesenja katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani, Mud Yusuph yu matatani kwa madai ya ubakaji wa denti wa darasa la kwanza,10,  (jina linahifadhiwa).
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya ofisi hiyo, mtuhumiwa huyo (55) alidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwake Kisarawe, Januari 20 mwaka huu.

Siku ya tukio inadaiwa mtoto huyo alikwenda nyumbani kwa mtumishi huyo ambaye ni shemeji yake. Mtuhumiwa ameoa dada wa binti.
Mtoto huyo alipofika kwa mtuhumiwa hakumkuta dada yake. Ikadaiwa mtuhumiwa aliitumia nafasi hiyo kumrubuni binti huyo kabla ya kumkamata, kisha akamvutia ndani na baadaye ikadaiwa alimbaka huku sebuleni kwake televisheni ikiwa inafanya kazi.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni juu ya tukio hilo, binti huyo alisema wakati akifanyiwa kitendo hicho alisikia maumivu makali na kulia, lakini mtuhumiwa alimtishia kumchinja endapo atapiga kelele.
“Baada ya kuniambia atanichinja nilinyamaza, lakini nilikuwa ninasikia maumivu, alipomaliza aliniambia nichukue maji nikanawe, baada ya hapo alinipa shilingi  elfu moja (1,000), nikaenda nyumbani.”
mtoto2
Mama mzazi wa mtoto huyo, Rehema Shukuru alipozungumza na gazeti hili alisema:
“Siku hiyo mwanangu alikuja nyumbani analia.  Nilipomuuliza analia nini, alinijibu shemeji yake amemfanyia kitu kibaya. Nilipomwangalia sehemu za siri nilikuta uchafu wa manii, ndipo nilipokwenda Kituo cha Polisi Kisarawe kutoa taarifa,” alisema.
Kwa mujibu wa mama huyo, mtuhumiwa huyo alitafutwa na kupatikana ambapo aliomba msamaha kwa kitendo alichokifanya lakini hata hivyo, polisi walimwweka mahabusu.
Wakati mtuhumiwa huyo akiwa selo, mtoto huyo alilazwa katika Hospitali ya Wilaya  Kisarawe kwa ajili ya matibabu, lakini katika hali ya kushangaza, siku mbili baadaye mtuhumiwa aliachiwa kwa dhamana na kuiacha familia katika mshangao.
Jitihada za gazeti hili kumfikia mtuhumiwa huyo ziligonga mwamba baada ya kutompata nyumbani kwake huku ikisemekana hayupo wilayani humo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kisarawe, Happy Ndosi alikiri kupokea taarifa ya mtoto huyo na kusema walimpima Ukimwi na kumpa dawa kama kutakuwa na maambukizi.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, SACP Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema taratibu zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa mazingira ya tukio lenyewe.

No comments:

Post a Comment