Kwa kawaida uvaaji wa mavazi hutegemea hali ya hewa au majira ya
husika ya mwaka. Ni muhimu kuzingatia majira ili kuepuka shida au
kukosa raha kwa kuchagua vazi lisilo sahihi.
Majira ya joto watu wengi hupata shida ya kuchagua
mavazi, kwani kipindi hicho huwa ni vigumu kwao kuvaa vizuri waendapo
kazini au kutoka kwa ajili biashara au shughuli zao nyingine.
Hata hivyo, kabla hujachagua kuvaa nguo, hata kama
ofisi yako ina utaratibu wa mavazi rasmi ya wakati wa joto, kumbuka
mavazi yako yana nafasi kubwa kwa mwonekano wako na hali ya joto haiwezi
kukubadilisha. Kumbuka kuwa huna sababu ya kuvaa nguo zisizofaa ili
kuepuka joto. Siku zote jiamini na hakikisha unapambana na joto ukilenga
kuonekana nadhifu.
Ufuatao ni mwongozo, ambao ukiufuata utakuwezesha
kufikia malengo yako ya kuonekana nadhifu kipindi cha joto, kwani
ukifanikiwa kuufuata vizuri, utaonekana mwenye kujua maana halisi ya
mitindo.
Unachotakiwa kufanya
* Vaa nguo zenye tabaka mbili, hii itakurahisishia
kubadilisha kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hapa unaweza kuvaa
blauzi yenye mikono mifupi au ‘top’ na jaketi jepesi ‘blazer’ au koti.
Hii itakurahisishia kuweza kulivua jaketi hilo au koti ikiwa utasikia
joto.
unaweza kuvua jaketi au koti lako na kubakia na blauzi au ‘top’.
* Jaribu kuvaa sketi badala ya suruali, hata kama
unapendelea kuvaa suruali, kwani sketi huruhusu hewa kuzunguka katikati
ya mapaja na kuondoa hali ya joto.
* Ili kuepusha usumbufu, hakikisha nywele zako
hazikugusi, hivyo ni vizuri ukazibana kwa mtindo utakaofanya zisiguse
shingo yako. Unaweza kuzikusanya katikati na kuzibana au kuzisuka.
Staili hizi zitafanya nywele zako zisikuguse shingo.
* Paka vipodozi vilivyo angavu, hasa ukiwa nje
kwenye joto kali. Joto kali na vipodozi vingi haviendani. Joto
husababisha vipodozi kuyeyuka na kuondoka, pia husababisha vitundu vya
hewa kuziba na ngozi kupasuka.
*Jipake manukato mazuri yanayoendana na majira ya joto. Manukato yenye harufu kali hunukia vibaya kwenye joto.
* Mavazi huendana na vitu vingine kama pochi,
viatu, mkanda, hata herein au mkufu. Unashauriwa kubeba pochi na kuvaa
viatu vyenye rangi angavu.
sichotakiwa kufanya
sichotakiwa kufanya
* Usivae ‘top’ isiyo na mikono kazini, hata kama una mikono mizuri.
* Usivae kaptula au sketi fupi, labda kama ni sare ya ofisi.
* Usivae viatu vya wazi. Vaa viatu vya kawaida, hasa vinavyofunika vidole .
* Epuka kuvaa rangi zinazowaka sana, unaweza kuvaa
nguo za rangi mbalimbali, lakini zisiwe rangi zinazowaka sana. Kumbuka ;
unataka watu wakuangalie wewe na siyo rangi ya nguo yako.
Usikubali kuharibu mwonekano wako kwa sababu ya
mabadiliko ya hewa, hakikisha kabati lako lina nguo zinazokwenda na
halijoto, wakati huo huo mwonekano wako unaendelea kufanana na taaluma
yako.
No comments:
Post a Comment