Mwanamke mmoja mfaransa (52) amejikuta mikononi mwa polisi
wa jiji la Paris katikati ya mwezi june, baada ya kukamatwa kwenye chumba cha
mtihani akimfanyia mtihani wa Kiingereza mwanae mwenye umri wa miaka 19, huku
akijiweka kisichana zaidi wasimshutukie.
Ripoti kutoka nchini humo zinasema mwanamke huyo
aliyejulikana kwa jina la Caroline D aliingia kwenye chumba cha mtihani akiwa
amevaa skin jeans na viatu aina ya Converse ili aonekane kama mwanae.
Lakini jicho makini la msimamizi wa mtihani lilimnasa mama
huyo kwa kuwa msimamizi alikua tayari alishamuona mwanae wakati anafanya
mtihani wa Philosophy, kwa hiyo akamshtukia mama huyo kwa muonekano wake na
sura yake ya kiutu uzima.
Msemaji wa Polisi wa Paris alisema mwanamke huyo alikiri
makosa yake ya udanganyifu na kusema kuwa kiukweli yeye alikuwa anaweza zaidi
Kiingereza zaidi ya mwanae.
Mwanamke huyo anakabiriwa na mashtaka ya udanganyifu na
anaweza kulipa fine isiyopungua £7,000.
No comments:
Post a Comment