WATOTO wawili wa familia moja wamekufa maji baada ya kutumbukia
kisimani walipokuwa wakichota maji wilayani Bunda, mkoani Mara.
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi, katika
Kijiji cha Changuge Kata ya Mcharo wilayani hapa, wakati watoto hao
walipokuwa wakichota maji kisimani.
Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Mcharo, Waziri Kingi aliwataja watoto waliokufa
maji kuwa ni Daud Makoye (4) na Raphael Makoye (2). Walikuwa wanaishi
nyumbani kwa Onesmo Mashenene mkazi wa kijiji cha Changuge.
“Wakati
Raphael akichota maji alitumbukia ndani ya kisima hicho, mkubwa wake
yaani Daud alipojaribu kumuokoa wote wakazidiwa maji na kupoteza
maisha,” alisema. Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Ferdinand Mtui,
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi bado
unaendelea.
hiki xio kisima halisi palipotokea tukio hilo,
No comments:
Post a Comment