Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka
Watanzania kuongeza juhudi za kuzuia maambukizi ya Virusi Vya
Ukimwi(VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili katika Tanzania iweze
kuwa na kizazi kisichokuwa na VVU na ugonjwa wa Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Kikwete
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa wadau wa kuzuia maambukizi ya VVU
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha mama Kikwete aliwataka Watanzania
kuchangia sh. 100 katika kupambana na tatizo kwa mchango utawapa nguvu
wadau wengine kuwaunga mkono.
Aliwataka wadau wamaendeleo kuendele kuunga mkno katika juhudi za kuondokana na tatizo hilo.
" Lazima juhudi za makusudi zifanyike
bila kuchoka kwa maeneo yote Serikali, NGO's, taasisi za dini mashirika
ya kiraia na watu binafsi . Hii itasaidia kunusuru kizazi chetu na kuwa
na nguvu kazi iliyobora, kizazi kisichokuwa na maambukizi na VVU na
Ukimwi," alisema Mama Kikwete huku akisisitiza Tanzania bila Ukimwi
inawezekana.
Aliongeza kuwa mikakati imara na endelevu
ni lazima iwepo kama vile kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU na
Ukimwi kwa kushirikisha jamii na kutoa tiba kikamilifu zinaweza
kupunguza maambukizi hayo.(P.T)
Alisema asilimia 98 ya wakina mama
wajawazito wanahudhuria kiliniki angalau mara moja na asilimia 43 mara
nne wakati wa ujauzito kati ya hao, asilimia 81 wanapimwa VVU.
Aliwataka wakina mama wajazito kuhudhuria
kiliniki wakati wa ujauzito kuanzia siku ya kwanza hadi
watakapoajifungua ili idadi ya wanahudhuria kiliniki iweze kufikia
asilimia 100.
Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Seif Rashid alisema hivi sasa Tanzania imefanikiwa kupunguza
maambukizi hayo kwa asilimia 15 mwaka 2012 kutoka asilimia 19 mwaka 2011
na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2015.
Alisema asilimia 90 ya wakina mama
wajawazito wamepimwa VVU kati yao asilimia 64 wamegundulika wanaishi na
VVU , pia asilimia 55 ya watoto wanapatiwa dawa za kupunguza makali ya
ugonjwa huo.(ARV's).
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara
hiyo , Dk .Neema Rusibamayilla alisema alisema awamu ya pili ya
kupambana na tatizo hilo itaanza Januari mwaka huu katika mikoa mingine
16.
Mratibu wa huduma hiyo kutoka Malawi, Dk.
Michael Eliya alisema ni muhimu kuweza katika utoaji wa huduma,
kuboresha miundombinu ,ikiwemo rasilimali fedha na watu katika
kufanikisha malengo hayo.
No comments:
Post a Comment