Sunday, 26 January 2014
NGONO,USAGAJI WASHAMIRI KATIKA SHULE MOJA YA SEKONDARI HUKO PWANI
Shule moja ya sekondari ya wasichana iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, imelalamikiwa na wanafunzi pamoja na wazazi kuwa mabinti wanajihusisha na vitendo vya ngono vya jinsia moja (usagaji).
Akizungumza na NIPASHE mmoja wa wazazi (jina linahifadhiwa) alisema shule hiyo imepoteza sifa kwa kuwa kuna wimbi kubwa la wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo vya usagaji.
Alisema mtoto wake alikuwa ameanza kidato cha kwanza mwaka jana na baada ya kumuandikisha ndipo baadhi ya watu walipomueleza kuwa shule hiyo kwa sasa ina sifa mbaya ya mchezo ‘huo mchafu.’
"Baada ya kuelezwa nikasema nitalifanyia kazi jambo hilo hivi karibuni katika kupekua madaftari ya mwanangu nakutana na kibarua cha mapenzi alichoandikiwa na msichana mwenzake niliumia sana na nilitumia nguvu kumbana bila hivyo asingeniambia," alisema
Alisema ilimbidi amhamishe binti yake na kujiunga na shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Tanga kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha pili mwaka huu.
Mzazi huyo alisema anashangazwa ni kwa nini hatua hazichukuliwi wakati suala hilo ni la hatari kwani watoto wao wataharibika kiakili pamoja na kimwili na wanaweza kuambukizana VVU na Ukimwi..
Alisema wakati mwanaye akisoma katika shule hiyo alikuwa akihudhuria vikao vya wazazi mara kwa mara na kwamba kila kikao walikuwa wakifukuzwa wanafunzi kutokana na mwenendo huo.
"Hili tatizo ni kubwa na kufukuzwa kwa mwanafunzi sidhani kuwa wanatatua tatizo nadhani hakuna usimamizi mzuri kwani wangeweza kudhibiti kwa haraka tatizo hilo kabla ya kuwa kubwa," alisema
Pia alisema ndugu yake imembidi amhamishe mwanae na kumtafutia shule nyingine kwa kuhofia binti yake kurubuniwa kwani wanakuwa ni wadogo na hawaelewi chochote, hivyo inaweza kuwa rahisi kudanganywa na kuingia kwenye vitendo hivyo viovu.
Alisema kuwa hata kiwango cha ufaulu kwa sasa shule hiyo imeshuka kutokana na tatizo hilo kwa wanafunzi .
Hata hivyo, NIPASHE ilizungumza na mwanafunzi mmoja ambaye anasoma katika shule hiyo kuhusiana na suala hilo ambapo alikiri kuwepo kwa jambo hilo na kueleza kuwa wanaofanya mchezo huo ni wa kidato cha tano na cha sita.
"Mimi hawajanifanyia ila najua wanaofanya mchezo huo ni wale walioko kidato cha tano na cha sita," alisema Pia kuna baadhi ya wazazi wengine wamekuwa wakilalamikia jambo hilo na kueleza kuwa ndugu zao imewalazimu kuwahamisha watoto wao kutokana na vitendo hivyo vinavyofanyika shuleni hapo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment