Thursday, 20 June 2013
Waziri Mkuu wa Tanzania ameruhusu Polisi wapige Raia
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda leo ameruhusu Jeshi la Polisi iendelee kudhibiti watu wanaokaidi amri halali ya jeshi hilo,kama sehemu ya Operesheni ya Jeshi wakati wa kukabiliana na watu wenye kuleta vurugu.
Pinda alitoa kauli hiyo jijini Dodoma katika vikao vya Bunge, wakati wa maswali na majibu ambapo alisema kwamba, Jeshi la polisi litaendelea kuwakabili na kuwadhibiti ikiwa ni pamoja na kupiga wale wote wanaokiuka amri ya Jeshi hilo.
"Jeshi la Polisi litaendelea kudhibiti watu wanaokaidi amri halali inayotolewa katika kulinda amani ya nchi iliyopo, liendelee kuwapiga Wananchi pindi wanapoonekana kwenda kinyume na sheria"alisema Waziri Pinda.
Waziri Pinda ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho upepo wa kisiasa bado haijatulia hususan katika Mkoa wa Arusha ambapo imetokea shambulio la kigaidi,huku Pinda akikiri kwamba bomu iliyotumika katika shambulio hilo limetengenezwa nchini China.
Hata hivyo Kauli ya pinda imepingwa vikali na watanzania mbalimbali waliotuma maoni yao katika mitanda ya kijami,ambapo walisema kwamba kauli ya Waziri Mkuu inaweza kuchochea vurugu na kufanya hali kuwa mbaya zaidi ya sasa.
Juzi Waziri Mkuu alikuwa mjini Arusha kutembelea majeruhi wa shambulio la kigaidi waliopigwa bomu Juni 15 mwaka huu, katika Mkutano wa Kampeni za chaguzi ndogo za udiwani, uliokuwa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.Katika shambulio hilo watu watatu walifariki dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment