Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa Internet
ni zawadi kwa dunia nzima kutoka kwa Mungu lakini akaonya kuwa matamanio
ya kutaka kuwasiliana zaidi kutumia Internet kunawatenga watu kutoka
kwa familia na marafiki zao.
Amewataka waumuni wa kikatoliki kujiunga na mfumo wa dijitali.
"Internet... inatoa nafasi ya mafanikio mengi. Hiki ni kitu kizuri bila
shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,'' alisema Papa.
Katika ujumbe wake kwa dunia nzima ambao hutolewa kila mwaka, Papa
amesema kuwa mfumo wa dijitali, unapaswa kuwa mtandao wa watu wala sio
nyaya tupu.
Papa mwenyewe ana akaunti kwenye Twitter ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni kumi.
Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu kukutana na kujuliana hali.
Kadhalika amewataka waumini wa kikatoliki kutodhani kuwa ni mawazo yao
na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati wakiwasiliana na watu wa dini
nyinginezo.
No comments:
Post a Comment