Habari za asubuhi wapendwa wafuatiliaji wa blog hii! kabla ya kuanza
mada hii ya leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu
kuweza kuniamsha salama nikiwa na afya njema.
Mada yangu leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.
Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya
utoaji mimba, utupaji wa watoto na hata kuwa na watoto wa mitaani
yanasababishwa zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa ambazo zingine
zinatokana na mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga.
Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo
iko katika makundi makuu matatu3 ambayo ni : mzunguko mfupi(siku25
kurudi nyuma), mzunguko wa kawaida(siku28) na mzunguko mrefu(siku30-35)
Wanawake wengi mzunguko wao huwa ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndio leo nitawaongelea zaidi.
NAMNA YA KUTAMBUA MZUNGUKO WAKO.
Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia
siku ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya
hedhi ya mwezi unaofuata, kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15
December basi hiyo ndio siku yako ya kwanza.
Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza
kushika mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi
siku ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.
Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?
Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa24 hadi
48 baada ya kujamiiana hivyo kama utafanya ngono tarehe 12 na yai
likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo
zitarutubishwa.
kwa leo tuishie hapo mpendwa mfuatiliaji ili kukuachia nafasi ya
kuchangia zaidi na kuboresha yale ambayo sikuweza kuelezea hapo.
No comments:
Post a Comment