Thursday 27 March 2014

KUNA NJAMA KUVURUGA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Pande mbili zinazopingana ndani ya Bunge Maalum la Katiba zimesema kuna njama ya kuvuruga Bunge. Kauli hii imetumiwa katika kuelezea hali iliyojitokeza jana wakati wa kikao cha Bunge hilo kuhusu mvutano wa mabadiliko ya kanuni.

Njama zinazoelezwa na pande hizo ni za kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya, zikirejea yaliyotokea jana jioni ikiwamo zomeazomea hali iliyomlazimu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kuliahirisha Bunge hadi leo jioni.

Baada ya kuahirisha Bunge hilo, Sitta alikutana na waandishi wa habari na kusema kwamba kuna njama za baadhi ya wanasiasa kutumia vurugu kuhujumu mchakato wa upatikanaji wa Katiba, badala ya kujenga hoja.
Bila kuwataja wanasiasa hao, Sitta alisema ikiwa hawataki kuendelea na mchakato huo, basi waondoke na kuwaacha wenye nia njema.

“Wanasiasa hawa wamedhamiria kuvuruga mchakato wa Katiba, tuhuma ambazo tumetuhumiwa leo na Lissu ni uongo na uzushi, mimi sihusiki na kupeleka marekebisho ya kanuni kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge,” alisema Sitta.

Sitta alikuwa anajibu mchango wa mjumbe wa Bunge, Tundu Lissu alioutoa mapema kwenye kikao cha jioni, akipinga kilichoelezwa ni njama za kutaka kubadili kanuni kinyemela ili kumsaidia mwenyekiti kulidhibiti Bunge.

Sitta alisema kwa kuzingatia kanuni ya 59 (1), Kamati ya Uongozi ina mamlaka ya kupeleka marekebisho ya kanuni ili kuliwezesha Bunge kufanya kazi vizuri.

Alisema hoja kwamba haiwezekani kufanyika mabadiliko hata kabla ya kuanza kutumika kanuni, siyo ya msingi kwani kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira yake.

“Kamati ya Uongozi ndiyo ilipeleka waraka wa mabadiliko ya kanuni kwa Kamati ya Kanuni na Haki kwa kuzingatia kanuni, lakini hata kabla ya kujadiliwa na kamati husika inaonekana kuna wajumbe ndiyo wameichukua na kuifikisha bungeni,” alisema Sitta.

No comments:

Post a Comment