Huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda mjini
Mombasa pwani ya Kenya ambapo magaidi walivamia kanisa siku ya Jumapili
na kuwapiga risasi waumini, mmoja wa waathiriwa wa shambulizi hilo
amefikishwa Nairobi mwa matibabu maalum.
Mamake aliyekuwa anamkinga kutoka kwa magaidi waliovamia kanisa hilo siku ya Jumapili ,alifariki kanisani humo baada ya kupigwa risasi. Inaarifiwa risasi aliyomuingia kichwani Cyprian ilitoka kifuani kwa mamake na kuishia katika ubongo wa mtoto huyo.
Mamake Cyprian, alikuwa miongoni mwa watu sita waliouawa katika shambulizi hilo, baada ya washukiwa watatu wa ugaidi kulivamia kanisa la Joy in Jesus katika mtaa wa Likoni na kuanza kuwafyatulia waumini risasi kiholela.
Cyprian atafanyiwa upasuaji maalum katika hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi.
Mtoto Cyprian Osinya na kakake walikuwa kanisani wakati wa shambulizi la Jumapili
No comments:
Post a Comment