Uganda imetoa tahadhari kwamba kundi la wanamgambo la
Al Shabaab linapanga kutumia malori ya mafuta kama mabomu katika
mahambulizi yao.
Kundi la Al Shabaab limefurushwa Mogadishu kutokana na juhudi za wanajeshi wa Muungano wa Afrika
Mkuu wa polisi wa Uganda,Kale Kayihura, amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba idara ya polisi na ujasusi zina taarifa za kuthibitishwa kuwa kundi la Al-Shabaab linapanga kulipua malori ya mafuta nchini Uganda na kusababisha uharibifu mkubwa.
Ameshauri wananchi kuwa waangalifu na waweze kutoa taarifa zozote kwa polisi.
Uganda na Kenya ziko na wanajeshi wake nchini Somalia kusaidia wanajeshi wa Somalia na wale wa Muungano wa Afrika kupambana na kundi la Al Shabaab.
Wapiganaji hao wamekiri kufanya mashambulizi katika nchi hizo mbili na kutishia mashambulizi zaidi ikiwa Kenya haitaondoa wanajeshi wake kutoka Somalia.
Kundi la Al Shabaab liliwaua watu 76 katika mji mkuu wa Uganda Kampala mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment