Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi
kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza
lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa
dhati.
Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana
hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye,
utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.
Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli
lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii
wameachika na bado wanaranda mtaani.
Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na
ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na
ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee
kwake.
Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi
ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo
nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.
Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au
kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.
Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango
kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo
lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.
Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna
wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila
wanachohitaji.
Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa kwani kwa hali
ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.
Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya wanawake ambao
wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao
furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.
Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya
ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana
lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama
magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu
kwa misingi ipi?
Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye
anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike
kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa
tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.
Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha
makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia
waume zao.
Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazooonekana
kuwashika waume za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na
wabunifu.
Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye
kama yale wanayofanya nyumba ndogo? Kuna dada mmoja nilizungumza naye hivi
karibuni akaniambia eti amenuniana na mumewe huu ni mwezi wa pili baada ya
mwanaume wake huyo kutaka afanyiwe mambo ambayo yeye aliona kinyaa kuyafanya.
Kabla ya kumjibu kwanza niliguna, sababu ya kuguna ni kwamba
niliyagundua hayo mambo ambayo aliona kinyaa kumfanyia mumewe. Niseme tu
kwamba, mapenzi wakati mwingine ni uchafu, wanaojua mapenzi wanajua kwa nini
nasema hivyo.
Nilichomjibu mwanamke huyo ni kwamba, kama mwanaume huyo
anampenda amfanyie kila atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa,
mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo
wengine wamekuwa wakiyafanya na wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.
Naomba niseme tu kwamba, huenda unajiamini kuwa ni mzuri na
umbo la kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua
bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi
mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.
Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo
atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatia.
No comments:
Post a Comment