Saturday, 9 November 2013

Njia za kuongeza ladha ya mapenzi na umpendaye

1.Toa milio ya kupendeza: Mlio ni tiba ya kushangaza. Utakuja kufahamu jambo hilo utakaposikia muziki ambayo unakufurahisha na ni dhahiri njia hii ni nzuri kwa kupumzika. Njia nyingine ya kuitumia mlio ni kuimba au kutoa sauti ya kawaida tu. Simama au kaa chini hali umefumba macho. Vuta pumzi ndani, fumba macho, pumua hewa nje na mlio wowote unaoona mzuri, utoe usikike. Fanya hivyo mara kadhaa.


2.Kuwa mtoto mdogo: Jilaze chini kwenye sakafu, jifanye ni mtoto mdogo kwa kurusharusha mikono na miguu na kujigeuza upande wowote unaodhania kuwa mzuri, toa kelele unayotaka kuitoa. Zoezi hili ni zuri sana kwa ajili ya kutoa hangaiko la moyo.


3.Tabasamu: Fumba macho jifanye kuwa ndani ya tumbo lako kunatabasamu na sasa linatembea kwenye uti wa mgongo wako. Na tabasamu hilo linaendelea kutembea hadi nyuma ya shingo yako na kusimama nyuma ya macho yako. Lione hilo tabasamu kwa muda kidogo. Halafu liache liingie machoni mwako na taratibu kusambaa usoni mwako. Wacha itokee hivyo, baadaye fumbua macho yako na kama unataka, wacha tabasamu lako liwe kicheko.


4.Jione upo salama: Njia nyingine ya kuondokewa na hofu ni kurudiarudia kusema, "Nipo salama." Kabla ya kukutana au kuanzisha mazungumzo na mtu yeyote yule.


5.Ikabili hofu: Kutakuwa na hofu kila siku, jiruhusu kuiona hofu na usisite, baadaye fanya hilo jambo ambalo lilikuwa linautia hofu, tumia nguvu kwa kusema, "ione hofu hata hivyo hutenda jambo hilo."


6.Kuwa katika hali ya mepenzi: Kumbuka wakati unaoupenda sana katika maisha yako, ione picha ya jambo lililokupendeza siku hiyo moyoni mwako. Zione hisia ulizozipata. Baadaye zisafirishe hisia hizo kutoka juu hadi chini ya uti wa mgongo wako huku ukivuta pumzi ndani na kupumua nje.


7.Eleza tatizo lako: Kama una tatizo ambalo unashindwa kulitatua lieleze tatizo hilo kwa watu wengine waziwazi. Jihisi unalichukia tatizo lako na unalitia ndani ya kikapu lilifungwa kwenye puto kubwa, halafu lirushe puto hilo angani. Litazame hilo puto likipotea angani


8. Kuwa unapenda: Kumbuka wakati uliopenda sana katika maisha yako. Litazame tukio kama vile unatazama sinema. Ijue hisia uliyopata ichukue hisia hiyo na kuleta wakati wa sasa, fanya kama vile hisia hiyo inasafiri kutoka juu hadi chini ya uti wako wa mgongo, hali ukivuta pumzi na kupumua.


9. Toa dukuduku lako: Kama una tatizo ambalo huwezi kulitatua sema tatizo lako kwa sauti, jifanye unalitia tatizo hilo lote ndani ya kikapu kilichofungwa kwenye puto kubwa, lifungulie hilo puto ili lipae hewani, liangalie linavyopotea mawinguni.


10. Jizoeshe kwa nguvu: Kuna ushauri wa aina nyingi kuhusu kujipa nguvu. Unaweza kutengeneza aina yako mwenyewe, hakikisha aina hizo ni sahihi.
Hapa chini ni baadhi tu ya aina za nguvu za kuzizungumza kila siku, kwa uzoefu wangu sio vizuri kuzidisha mara elfu moja kwa siku.
a)Najipenda kama nilivyo.
b)Najikubali kama nilivyo.
c)Najiheshimu kama nilivyo.
d)Mimi ni mtu mzuri ipasavyo.
e)Nina nguvu za kutosha kufanya yote ninayotaka kufanya (ni vizuri kusema hivyo wakati ukiwa umechoka)
f)Napaswa kupendwa.
g)Napenda kuwa na nguvu za kupenda.
h)Napenda kupendwa sana


11: Dhibiti fikra zako:
Kuwa mwangalifu na fikra zako wakati huwezi kuacha kufikiria kuhusu kitu au mtu. Jipatie sekunde 30 kuendelea kufikiria fikra hizo hizo, baadaye sema kwa sauti ukizidisha sauti inakuwa vizuri sana 'wacha'.


12: Badilisha 'Napaswa':
Tazama mara ngapi unatumia neno 'napaswa' au 'nawajibika'. Badilisha maneno hayo kuwa 'kama nataka kufanya kitu naweza.'


13: Jipende wewe mwenyewe:
Kaa uchi wa nyama mbele ya kioo, tafuta neno zuri la kusema kuhusu mwili wako, "Sina kasoro.


14: Jikumbatie mwenyewe:
Fumbua macho, nyoosha mikono yako mbele yako, vuta pumzi, fumba macho uvingirishe mwili wako kwa kutumia mikono yako, pumua taratibu halafu tazama.


15: Kama unawaona watu na kuwaza uwaambie; "Jiambie mwenyewe, "Nipo salama", epukana nao.


16: Je, ungekuwa sawa au ungekuwa na furaha? Kuwa msikilizaji mzuri, msikilize patna wako bila ya kipingamizi.


17: Ulivyo haswa:
Mazoezi yote hayo yatakusaidia kuwa kama ulivyo haswa, ulivyo haswa kunataka uwe na amani, furaha, mapenzi ya kutosha na pia kujua namna ya kuvipata vitu hivyo.
****
Njia zingine za kuimarisha kimapenzi
*Je kuna umuhimu gani kwa wapendanao kuoga pamoja?
Bila shaka watu wengi wamekuwa wakijiuliza swali hili leo nitawaeleza ukweli kwani siku zote lengo langu ni kuhakikisha kuwa wapendanao wanaendelea kudumisha urafiki wao.


Ni kweli kuna baadhi yetu wanaogopa kuoga na wapenzi wao kutokana na sababu wazijuazo wao wenyewe, lakini ni vema wakajua kuwa kwa woga wao huo ni sawa na kulikimbiza penzi. Nasema hivyo kwa kuwa naelewa kuwa kuoga pamoja na mpenzi wako kunaongeza na kuimarisha zaidi mapenzi kati yenu.


Jamani hivi ni nani hapendi kusuguliwa taka za mgongoni na mpenzi wake? Ni raha iliyoje? Kama hujafanya, basi jaribu siku moja, kila siku utataka uoge pamoja na mhibu wako. Ni jambo linaloeleweka kuwa mikono yako mwenyewe huwa haifiki maeneo ya katikati ya mgongo ambapo ingeweza kusugua taka za maeneo hayo.


Hivyo ni muhimu wakati unapokwenda kuoga muombe mpenzi wako ukaoge pamoja. Msuguane taka mnavyotaka na kuhakikisha kuwa maeneo hayo ya mgongoni yanakuwa safi.


Manufaa mengine yatokanayo na kuoga pamoja na mpenzio ni hali ya kuusanifu vizuri mwili mzima wa mwenzio. 


Kwa kuwa kila kiungo chake mwilini kitaonekana kwa kuwa wazi zaidi, na hivyo kukuletea burudani ya aina yake pamoja na msisimko wa kupindukia.


Wapendanao wanapoingia bafuni kuoga inabidi kila mmoja amsuuze vizuri mwenzake na kumsugua taka hasa maeneo yale niliyosema ambako mkono wao si rahisi kufikia. Kwa kufanya hivyo hakuna ubishi kila mara mtapenda muoge pamoja na mpenzi wako.


Lakini pamoja na uzuri wa kuoga pamoja na mwenzako, ni muhimu wapendanao kama wanaishi nyumba yenye wapangaji basi wa si jambo la busara ikiwa mtatumia muda mwingi huko bafuni, kwa sababu kwa kufanya hivyo mnawakarahisha wengine wanaotaka kutumia bafu.
Ogeshaneni haraka haraka na kisha muondoke kuwapisha wenzenu walitumie hilo bafu pia.


Ni kitu kinachoeleweka kuwa kwa kuuona mwili wa mpenzio ukimeremeta ukiwa mtupu huko bafuni kunaweza
kuamsha hisia zingine za kuvamiana kimapenzi, lakini si vizuri hisia hizo mkajaribu kuzituliza huko huko. Kama itatokea unaona mwenzako au wote wawili mmezidiwa na hisia za mapenzi, humo bafuni, basi ni muhimu mkajimwagia maji haraka haraka na kurudi chumbani ili kuzituliza hisia zenu.


Nasema hivyo kwa sababu imeshatokea mara kadhaa kwa baadhi ya wapendanao baada ya kuoga pamoja huko bafuni wanashindwa kujizuia na kuamua kumaliziana huko huko bafuni.


Hilo jambo halifai kwa vile kuna watu pengine wanasubiri kuingia humo bafuni kutawafanya wanaosubiri kulitumia bafu wasote kwa muda mrefu zaidi. Kwa kuwa itawalazimu wapendanao watumie muda wa ziada huko bafuni, kushughulika na hicho kitu walichokuwa wamekianza.

No comments:

Post a Comment