Thursday, 25 April 2013

HAKUNA ALIYEKAMILIKA VUMILIANENI UDHAIFU WENU, MTADUMU KWENYE MAHUSIANO YENU........


Udhaifu maana yake ni nini?

Ni tabia ya mtu yenye upungufu katika matendo yake ambayo kwa njia moja au nyingine inawakwaza wengine.
Kwa nini udhaifu huwa kero?
Kama nilivyosema awali, upungufu katika tabia ya mtu hutokana na mazingira au malezi aliyokulia, hivyo kuwa tofauti na mwingine. Katika mapenzi kumekuwa na matatizo mengi ambayo yamekuwa kero kubwa, mengine yamevunja uhusiano.
Mada yetu ya leo
Katika maisha kila mwanadamu ana tabia yake ya asili tofauti na ya mwenzake, kutokana na mazingira au malezi aliyokulia. Wengine wana kiburi, wakimya, waongeaji sana, wabishi, wapenda kudeka na wasiopenda kufanya kazi ngumu. Watu wengi wamekuwa wakiteswa na tabia  za wenza wao, hasa wanaume. Unaweza kuwa na mpenzi au mke ambaye hayupo makini nyumbani, hali hii hukukwaza kwa kuwa hukuizoea..
Vitu ndani vinakuwa shaghalabaghala, akiamka hafanyi usafi au anafanya muda atakaojisikia. Mtu akija ghafla atafikiri nyumba haina mwanamke na kama kuna mtoto mdogo, kila kona inanuka mkojo.
Inakuwa tofauti kwa mwanaume akienda kwa rafiki yake anakuta nyumba safi mpaka anaona raha, lakini kwake hakai hata dakika tano, harufu ya mkojo inamkimbiza.
Wengine kitandani maudhi matupu, akiambiwa geuka au tubadili mtindo wa mapenzi, yeye anaona usumbufu. Inakuwa tofauti na akikutana na mwanamke wa pembeni anayeelewa na si mbishi, anajikuta akimchukia mkewe au mpenzi wake na kuamini hafai kwa vile ni mbishi na si muelewa, mtu asiyetaka kujifunza.
Nina imani yapo mengi ambayo yamekuwa kero ndani ya uhusiano na kukufanya ulichukie penzi lako. Kama nilivyoanza kueleza mwanzo kuwa tabia za watu hutofautiana zipo zinazobadirika kulingana na mazingira.
Lakini zingine huwa kama kilema, huwa hazibadiliki na kuwa maudhi ambayo huchelewa kukoma, huo ndiyo udhaifu wa mwenzako.
Inawezekana ukawa unakuudhi sana na kujikuta ukipata wazo baya juu ya mwenzako, hata kutafuta mtu wa pembeni ambaye anakuwa ndiye mtu sahihi kwako.
Nataka kuwaambia tatizo ndani ya nyumba halimalizwi nje ya nyumba bali ndani ya nyumba. Tabia ya mtu aliyokuwa nayo ni vigumu kubadilika mara moja, ndiyo maana inaelezwa ni muhimu kuvumiliana huku tukijitahidi kurudishana katika mstari.
Kama umegundua udhaifu wa mwenzako hupaswi kumtenga au kutafuta suluhisho nje ya nyumba, bali unapaswa kumrekebisha huku ukimvumilia. Kaa naye, mweleze matatizo yake ambayo yanakukwaza na kukukosesha amani ndani ya penzi letu.
Nawe unapoelezwa udhaifu wako badilika kwa kuondoka katika tabia yako ya zamani. Ulizoea kupikiwa, kufuliwa na hujawahi kushika ufagio, pia ni mgeni wa mapenzi, unatakiwa kuugundua udhaifu wako kupitia kwa mwenzako.
Inawezekana kabisa umezoea mapenzi ya kifo cha mende lakini umeolewa na kukutana na staili zaidi ya mia, usiwe mbishi eti hujazoea.
Jifunze taratibu ili umfurahishe mpenzi wako, siri ya mapenzi ni kulifanya lile linalomfurahisha mpenzi wako na kuliacha linalomuudhi. Kwenda kinyume ni kulivunja penzi lako kwa mikono yako mwenyewe.
Pamoja na kuvumiliwa upungufu wako, unatakiwa kubadilika, kwani hakuna mtu anayevumilia maudhi ya kila siku, akichoka hana msalie mtume. Lakini tofauti na hivyo, ukiachwa utakuwa mchawi mwenyewe.

No comments:

Post a Comment