Thursday, 25 April 2013

MAALUMU KWA WALE WANAWAKE WANAOTAKA KUOLEWA,Soma zaidi hapa........................

HATA kama utapingana na jambo hili, lakini ukweli utabaki palepale; kila jinsi inahitaji sana kuungana na jinsi nyingine katika tendo muhimu na la kihistoria katika maisha liitwalo ndoa! Yes, huu ni ukweli ambao upo wazi na utaendelea kusimama kama ulivyo.

Jinsi zote zina umuhimu na jambo hili, lakini kuna tofauti kidogo, kwamba mwanamke anasuburi kufuatwa na mwanaume, wakati mwanaume anaamua kumfuata mwanamke anayemtaka na kwa wakati wake.
Kuna kitu nataka kuweka sawa hapa, kwamba wanaume ndiyo huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume husika.
Wanawake wa ‘mjini’ huwa hawakubaliani na hili, kutokana na huu utandawazi unaohubiriwa siku hizi ikiwa ni pamoja na ‘kampeni’ za usawa zinazotetewa na wanaharakati wanawake, akinadada nao huchangamkia kueleza hisia zao kwa wanaume. Nadhani si jambo baya, ingawa linaweza kupokelewa kwa hisia tofauti na kila mwanaume kulingana na malezi au makuzi yake.
Hoja kubwa na ya msingi hapa ni jinsi gani mwanamke anaweza kuolewa haraka na mpenzi wake. Ikumbukwe kwamba, hapa nazungumza na wanawake ambao tayari wapo katika uhusiano, lakini wenzi wao hawana habari kabisa na mambo ya ndoa.
Nazungumza na wanawake ambao wapo kwenye uhusiano ambao haueleweki, lakini ndoa wanaitaka. Unajua cha kufanya? Twende pamoja.
EPUKA MAKUNDI
Mwanaume anapenda kuwa na mke mwenye staha, ambaye hana tabia za hovyo. Kuwa na makundi ya ‘mashangingi’ ni alama ya kwanza kabisa kuwa unapenda au tayari una tabia za kishangingi. Wanaume wengi hawapendi kabisa wanawake wenye tabia za hovyo, wenye kampani ambazo si nzuri.
Lakini yawezekana, jamaa alishakuambia juu ya kilio chake hiki, lakini wewe umekuwa kama umeweka pamba masikioni mwako, hili ni tatizo. Linda heshima yako, kaa mbali na makundi  hatari, ili umfanye jamaa akuone wewe ni mwanamke thabiti ambaye huigi, hushabikii na wala huna tabia mbaya. Utaonesha hili kwa kukaa mbali na makundi ya wanawake hatari!
MAVAZI
Kila mtu anamjua mtu wake alivyo, mwanamke hata wewe unamjua mpenzi wako alivyo. Sina shaka unafahamu anapenda nini na nini anachukia. Lakini pamoja na kwamba jamaa anaweza kuwa na vitu ambavyo vinamvutia zaidi, hata wewe kama mtoto wa kike, una mapendekezo yako au vitu ambavyo unapenda zaidi kuvifanya!
Huzuiwi, lakini swali la msingi ni kwamba, mwenzi wako anapenda? Kama wewe unapenda sana skin jeans (suruali za jinzi za kubana) na top (blauzi fupi) inayoacha kitovu nje, yeye hapendi kwa sababu ana nia ya kukufanya mke hapo baadaye, muelewe!
Sasa utakuwa mke gani ambaye kila mwanaume anaona sehemu zako za faragha hadharani?
Wanaume wengi hawapendi mambo haya hasa kwa wanawake ambao wana nia ya kuishi nao katika ndoa. Ukiachana na chaguo la mwenzi wako, lakini lazima wewe mwenyewe kama mwanamke wa mtu, ujitambue! Jisitiri vyema.
Kwani kuna urembo gani wa kuvaa nguo inayoonesha mwili wako? Kuna burudani gani kuacha nyeti zako wazi? Unataka nani akuone ulivyo? Mke hana sifa hiyo dada yangu, sasa ili uweze kuwa na sifa hii muhimu, lazima uzingatie sana mavazi yako.
USIJIKATISHE TAMAA
Hili nilishawahi kulizungumzia sana, baadhi ya wanawake wamekuwa wakikatishwa tamaa na rafiki zao au watu wengine wanaowazunguka, eti hawana hadhi ya kuolewa au watahangaika sana kupata mume, kisa eti hawavutii!
Mwingine anajinyima mwenyewe nafasi akisema; “Mimi nina balaa, sina bahati ya kuolewa, ndiyo maana wadogo zangu wote wameolewa nimebaki mimi.”
Huu ni uvivu wa kufikiri. Lakini dada yangu, habari iliyo njema kwako ni kwamba, ndoa unaitengeneza wewe mwenyewe. Unaitengeneza kwa misingi ya kwanza; kujipa moyo kwamba wewe ni mzuri na una sifa na haki za kuolewa kama wanawake wengine. Jipe moyo, huna nuksi wala balaa, wewe ni mzuri na una sifa za kuwa mke.
Iko hivi, ukianza kujishusha ni dhahiri kwamba hata mavazi yako hayatakuwa mazuri, uso wako hautakuwa na tabasamu na wala hutakuwa na matumaini moyoni, hapo ndiyo mwanzo wa kudhoofu afya yako. Utapata mchumba kweli? Utasubiri sana kwa mtindo huo!
USIWE NA PAPARA
Haizuiwi kuuliza kuhusu mustakabali wa uchumba wenu, lakini ni vizuri basi kuwa na kiasi. Kuuliza kila wakati au kuwa mtu wa kulaumu, hakutasaidia kumfanya jamaa achukue uamuzi wa haraka wa kukuoa na badala yake anaweza kupata picha tofauti.
Ni rahisi kuwaza kwamba, unachohitaji kwake ni ndoa na baada ya hapo hutakuwa na staha tena. Kuwa mjanja, achana na papara. Usilogwe ukamfanyia jambo zuri mpenzi wako, halafu ndiyo umuulize: “Sasa honey, mbona hata huzungumzii ndoa yetu? Hivi utanioa kweli? Niambie basi mpenzi wangu…”
Dada yangu, ukifanya hivyo, utampoteza! 

No comments:

Post a Comment