IMEELEZWA kuwa, licha ya matokeo ya kidato cha pili kutolewa `kimyakimya’ kupitia ofisi za Elimu za Kanda na kubandikwa shuleni, hatua hiyo haimaanishi kuwa waliofeli wamenusurika kutorudia darasa.
Hayo yameelezwa na Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu alipozungumza na gazeti la Habari leo jana.
Alisema kwa sasa Wizara inaendelea kujumuisha matokeo hayo katika ngazi ya Kanda kabla ya kutangaza rasmi idadi ya waliofaulu.
Alisema
kwa kawaida matokeo hayo hutangazwa na ofisi za elimu kanda na si Wizara
ya Elimu, lakini kuanzia wiki hii shule zimepata matokeo yao katika
ofisi za kanda. Jumla ya wanafunzi 531,457 walitajwa na Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi mwaka jana kuwa walitarajiwa kufanya mtihani huo.
No comments:
Post a Comment