Monday, 29 April 2013

Alex Masawe kushtakiwa kwa kesi ya mauaji...................



Mfanyabiashara maarufu, jijini Dar es Salaam, Marijani Msofe 'Papa Msofe', akiongozwa na Askari Polisi na Magereza kuingia kwenye chumba cha Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusomewa shitaka la mauaji ya Onesphory Kitoli, mahakamani


WAKATI Kesi inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Abubakar Marijani ‘Papaa Msofe ikiendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mfanyabiashara mwingine maarufu Alex Massawe aliyekuwa akisakwa na Askari wa Polisi Afrika Kusini amekamatwa.
Mfanyabiashara huyo aliwekewa mtego  na Polisi wa Afrika Kusini ambao wamekuwa wakimsaka baada ya kuombwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) ili akamatwe na kurejeshwa nchini.
Mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kwa kosa la mauaji baada ya kutajwa mahakamani Aprili 4, mwaka huu  katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6, 2011 akiwa nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo ambayo mshtakiwa wa kwanza ni mfanyabiashara maarufu, Abubakar Marijani ‘Papaa Msofe’, mshitakiwa mwingine, Makongoro Joseph Nyerere alitoa malalamiko, mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome mara baada ya Wakili wa Serikali, Mwanaisha Kombo kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe mpya ya kuitaja.
Chanzo cha habari hii kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania ililipasha gazeti moja la kila siku nchini Tanzania kwamba “Unajua kuna mlolongo wa taratibu za kutekeleza ili Massawe akamatwe. Kwanza lazima Polisi wa Tanzania watoe tangazo kwa Interpol juu ya kumsaka mtu huyo ili aletwe. Ndiyo maana Polisi wa Tanzania hawawezi kuzungumza chochote hadi watakapomweka mikononi mtuhumiwa huyo,” kilieleza chanzo cha gazeti hilo.
Hata hivyo habarimpya.com imehabarishwa na vyanzo vya ndani ya Jeshi hilo kwamba pamoja na madai kukamatwa kwa mfanyabishara huyo nchini Afrika Kusini bado hawezi kuletwa nchini kwa sasa mpaka serikali ya Tanzania na Afrika Kusini zitakapo toa kibali cha kusafirishwa kwake.

No comments:

Post a Comment