Kada wa CCM Hussein Bashe..
KADA CCM Hussein Bashe amekuwa mwanachama wa kwanza kujitokeza hadharani na kukemea tukio la kukamatwa kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema.
Katika taarifa yake iliyonaswa na waandishi wa habari Bashe anasema kwamba tukio la kuuwawa kijana wa Chou cha Uhasibu na matokeo yake kuishia kukamatwa Mbunge huyo.
"Badala ya kutafuta wauwaji kunatengenezwa mazingira ya kuleta vurugu (Instabillity) kwa kumkamata Lema, Kaka yangu Mkuu wa Mkoa Magesa Mulongo katika hili alivolisimamia na kulitekeleza ameonyesha udhaifu wa hali ya Juu"alisema Bashe katika taarifa yake na kuongeza.
"Matokeo yake inavunjia heshima Serekali ya Chama chetu na Kuongeza chuki dhidi ya CCM. Hakukua na sababu ya kuchukua maamuzi kwa jinsi alivyofanya (Kubahave 'the way he did') pale chuoni,alionyesha kiburi hakua msataarabu (humble) ,hakutumia Busara katika jambo hili".
Katika taarifa hiyo ambayo baadaye nakala yake ilipatikana katika mtandao wa Facebook Bashe aliendelea kufafanua kuwa Pale Chuoni kuna kijana ameuwawa,na yeye ndie Rais wa eneo lile tabia (attitude) alionyesha hakukua na uongozi (leadership) pale,tunakabiliwa na uchaguzi na kuna mtu ameuwawa na si tukio la kwanza, ila nguvu iliyotumika kumkamata Lema hazikusitahili.
Leo CCM mkoa wa Arusha wanakabiliana na maswali mengi kuliko Majibu,inasikitisha viongozi wanaotuwakilisha kuongoza ndio hao tunawaona Bungeni,ndio hao Kina Mulongo na maamuzi na attitude ya kaka Mulongo.
No comments:
Post a Comment