Monday 22 April 2013

Kenyatta ampa Odinga,Kolonzo ulinzi mkali


Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Rais Raila Odinga.


SIKU chache baada ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kukutana na Waziri Mkuu wa zamani wa nchini Raila Odinga na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo usala wao, Kenyatta ameamua kuwarejeshea viongozi hao vikosi vya ulinzi katika makazi yao.
Viongozi hao walisitishiwa ulinzi na kupokonywa magari ya serikali waliokuwa wakitumia siku cha baada ya Rais Kenyatta kuapishwa, wakati  viongozi hao wakiwa nchini Afrika Kusini kwa mapumziko.
Katika kuonyesha kwamba Rais Kenyatta ameamuwa kuwalinda viongozi hao kutoka muungano wa Chama cha CORD tayari Mkuu wa idara ya huduma za umma Francis Kimemia ameshapewa agizo la  kuandaa utaratibu utakaotumika kuwalinda viongozi hao wa CORD.
Awali Iluku ya nchi hiyo iliondoa askari wapatao 80 pamoja na magari ya serikali yaliyokuwa yakitumiwa na Odinga pamoja na Kalonzo, wakiwa nchini Afrika Kusini na hata waripo rejea nchini humo wakalazimika kutumia vyombo  binafsi vya ulinzi na usalama.
Raia na Kalonzo walikuwa wapinzani wakubwa wa Uhuru na makamu wake William Ruto katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliomalizika Machi 4 mwaka huu.
Baada ya uchaguzi huo Tume uhuru ya Uchaguzi isiyokuwa na mipaka Mipaka (IEBC) iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Ahmed IsaackEIBC kumtangaza Kenyatta kuwa Rais CORD walikiimbia Mahakama ya Juu ya nchi hiyo kupinga matokeo lakini Mahakama hiyo baada ya kusikiliza kesi hiyo ikitangaza kwamba Kenyatta ni Rais halali wa nchi hiyo.
Baada ya uamuzi huo wa Mahakama Odinga na Kalonzo walijitokeza mbele ya vyombo vya habari na kutangaza kwamba wamekubaliana na uamuzi wa mahakama hiyo huku wakiwataka wakenya kuungana na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya uchumi wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment