Kwikwi siyo neno geni katika masikio ya wengi, ingawa wengi wetu hupata tatizo hili, bila kujua sababu zake.
Pengine kwa kutojua sababu hizo baadhi tunaendelea kushikilia imani za kale kuwa ukipata kwikwi, basi kuna mtu anakusema.
Kutokana na hewa kuingia kwenye mfumo huo kwa
ghafla, kisanduku cha sauti hufunga hivyo kusababisha usumbufu kwenye
kiungo kidogo kama utando, kinachotenganisha mapafu na tumbo.
Mbali na hewa, yapo mambo kadhaa yanayochangia
kupata kwikwi, ambayo ni pamoja na; kula chakula haraka haraka na hasa
kama ni kikavu, kucheka sana na kwa muda mrefu, kula vyakula vyenye
viungo vikali hasa pilipili kali kama hukuizoea.
Kumeza vitu vya moto sana na kunywa pombe kupita
kiasi. Sababu hizi zinaweza kuchangia hewa kuingia kwa ghafla kwenye
mapafu na kusababisha kisanduku cha sauti kufunga.
Sababu nyingine za ugonjwa huo, zinahusiana na
mishipa ya fahamu iliyo na uhusiano na kiungo kinachotenganisha mapafu
na tumbo la chakula. Nyingine magonjwa ya homa ya mapafu (pneumonia).
Pia kuna baadhi ya madawa ambayo yakimezwa husababisha kwikwi.
Matibabu ya kwikwi ni ya kawaida.
Ikiwa inatokana na hewa kuingia kwenye mapafu ghafla inaweza kuisha yenyewe baada ya muda mfupi.
Mbinu zinazosaidia kupunguza kwikwi ni pamoja na;
kunywa maji ya baridi kwa njia ya kugugumia, kumtisha mtu mwenye kwikwi
japo siyo vyema kumtisha sana na hasa kama hujui afya yake vizuri.
Unaweza kumtisha mtu akazimia, hata kupoteza
maisha kama alikuwa na magonjwa mengine kama ya moyo. Vitisho visiwe
vikali, wala vya kisheria kama kumtishia mtu kumuua, kwani anaweza
akakupeleka mahakamani hata kama ulifanya hivyo kwa nia njema. Njia
nyingine ya kukata kwikwi ni kula sukari, hasa ukiiweka chini ya ulimi,
kubana pumzi kwa muda, kuchuchumaa na kuhakikisha magoti yamebana
kifuani, kung’ata limau na kadhalika. Katika kutibu kwikwi inayotokana
na magonjwa mengine ni muhimu madaktari kufanya vipimo na kutibu tatizo
husika. Mara nyingi kwikwi inapokaa kwa muda mrefu madaktari watampa
mgonjwa dawa za usingizi na zile za kupunguza msongo wa mawazo.
No comments:
Post a Comment