Monday 22 April 2013

KWA WALE WANAOTAKA KUWA NA NGOZI YENYE AFYA BORA,Hizi hapa njia 5 muhimu zitakazokusaidia kuwa na ngozi yenye afya bora........



Wanawake wengi hupenda kuwa na mvuto katika ngozi yao, hasa maeneo ya usoni mikononi na miguuni, basi njia hizi chache nilizoziandaa hapa kwaajili yako wewe unayependa kuwa na ngozi yenye afya, zitakufaa sana.

Kwanza safisha uso wako kwa maji na sabuni angalau kwa siku mara mbili. Osha kwa maji yenye joto, kwasababu maji ya moto hufungua vijitundu vilivyoko kwenye ngozi na maji ya baridi hufunga vijitundu hivyo vya ngozi, hivyo ni vyema ukaosha kwa kutumia maji ya joto pamoja na sabuni, kisha kabla ya kupaka makeup, pitisha maji ya baridi tena ili kuepusha ngozi kudhurika na hali ya hewa. 

Hakikisha unapunguza matumizi ya vipodozi haraka iwezekanavyo, kwani huziba vijitundu vya ngozi vinavyofanya ngozi kupumua. Usipake vipodozi wakati wa kulala, labda vile ambavyo ni maalu kwaajili ya ngozi. Lakini kwa ushauri unatakiwa kuoondoa vipodozi vyoote katika ngozi yako kabla ya kulala.

Unapaswa kuweka nywele zako nyuma na usitumie mikono mitupu wakati unapaka creame usoni, tumia vifaa maalum vya kupakia vipodozi.

Kula mlo bora, kumbuka kujumuisha matunda fresh na mboga za majani katika mlo wako. Matunda na mboga za majani huongeza vitamini A na vitamini E mwilini ambavyo ni vyanzo mojawapo vinavyoweza kuipatia ngozi yako muonekano mzuri na imara.

Kwa haya machache umeweza kuona kwa kifupi tu jinsi ya kuhifadhi ama kutunza ngozi yako ya uso ili kuipatia muonekano halisi wa ngozi yako.

No comments:

Post a Comment