NAMNA YA KUPIKA DAGAA+NYANYA CHUNGU+NAZI: RURAL OR URBAN STYLE
Hawa ni wale dagaa wa kigoma lakini wadogo wadogo sana, wachambue vizuri kwa kiasi utakacho kupika, halafu uwaoshe vizurii wasiwe na michanga.Andaa kitunguu, nyanya, carrot, hoho, ndimu na nyanya chungu, bila kusahau tui la nazi.
Weka mafuta kidogo sana kwenye sufuria kwakuwa mboga yetu tunaweka nazi, yakipata moto weka dagaa zako ulizozisafisha vizuri, zigeuze geuze halafu weka maji ya ndimu uliyokamua, geuza geuza moto usiwe mkali sana, katia kitunguu, endelea kugeuza hadi uone vitunguu vinageuka rangi na kuwa brown, halafu weka nyanya ulizokatakata ukachanganya na hoho na carrot, funika kwa muda kidogo inategemea na wingi wa mboga yako, ukifunua nyanya zitaanza kulainika ukigeuza utaona zinachanganyika na dagaa kuashilia zinalainika.
Kabla hazijalainika sana, weka nyanyachungu kwa juu ulizokatakata ukubwa uutakao, kwakuwa nyanya huwa zina maji mpaka hapo unakuwa hujaweka maji, ila ukiona mboga inashika chini, weka maji kidogo, funika, baada ya muda funua geuza geuza, weka chumvi kiasi, yale maji yakianza kukauka na kwakuwa nyanyachungu hazitakiwi ziive sana na kulainika sana weka tui lako.
Ukiweka tui la nazi acha ichemke vizuri, chumvi iwe ya kutosha isizidi sana maana chumvi ikizidi ni matatizo, utakuwa umeridhika imeiva ipua.
Na hii ni mboga yetu ikiwa tayari kuliwa na wali, ugali, ndizi za kuchemsha, mihogo ya kuchemsha, viazi hali kadhalika, ni tamu sana.
Ukishakula, baada ya nusu saa, shushia matunda yako bila kusahau maji ya kunywa, unamshukuru Mungu kwakukujalia msosi kama huu, unawaza next meal itakuwa ni chakula gani.
Msosi huu umeangalia mtu wa kawaida kabisa na aishiye mazingira yeyote either mjini au kijijini na mahali ipatikanapo nazi, na ni mboga ya kupika kwa muda mfupi sana,mpishi ni mimi mwenyewe
No comments:
Post a Comment