Mama wapya kila siku wanawaza ni jinsi gani wataweza kuwalea watoto wao, hasa inapofika wakati wanatakiwa kuwalikiza vyakula zaidi ya maziwa ya mama. Swali kubwa linakuwa ni aina gani ya chakula wapewe watoto.
Kwa miezi 4 mpaka 6 ya mwanzo mtoto huwa anajitosheleza na maziwa ya mama kwa lishe au hata wakati mwingine katika maziwa ya kopo kwa wale wasionyonyesha. Kwa wakati huo mama anakuwa na uhakikika wa chakula kinachomtosheleza mtoto wake na upatikanaji wake.
Lakini baada ya miezi 6 na kuendelea mtoto anahitaji zaidi ya maziwa, hapo ndipo unatakiwa umpatie chakula zaidi. Lakini kwa mama ambaye ndio kwanza unalea kwa mara ya kwanza, ni kipindi kigumu sana na cha mashaka makubwa kwani hujui ni chakula gani umpatie mwanae.
Lazima umpatie vyakula vyenye lishe bora.
Vyakula vyenye madini ya chuma ni muhimu sana katika ukuaji wa mtoto, madini ya chuma husaidia uzalishwaji wa haemoglobin( sehemu za chembechembe nyekundu za damu ambazo zinabeba oxygen mwilini), vile vile madini ya chuma yanasaidia ukuaji wa ubongo wa mtoto, mfano mtoto kuwa na kumbukumbu nzuri. Hivyo ni muhimu kumpatia mtoto vyakula vyenye madini ya chuma kila siku.
Vyakula hivyoni kama , nyama ya ngombe,kuku, samaki,mayai ,parachichi, broncoli na spinach.
Vyakula vyenye madini ya zinki.
Kama ilivyo kwa madini ya chuma zink pia husaidia ubongo wamtoto ukuwe vizuri na katika speed inayotakiwa. Zink inasaidia celli za mwili kukuwa na kujiimarisha zenyewe kupambana na magonjwa. Kama kawaida vyakula vyenye madini ya chuma pia kwa asilimia chache vina madini ya zinki, Vyakula kama Nyama,kuku,samaki.
.
Vyakula vya madini ya Calcium na Vitamini D
Calcium ni muhimu kwa kuwa na mifupa imara, na vitamin D husaidia na ni muhimu pia.Maziwa ya mama kwa miezi ile ya mwanzo yamesaidia upatikanaji wa madini hayo ya calcium kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kwa upande wa Vitamini D, Doctors wameshauri kuwapatia watoto supplements kwa sababu kuna vyakula vichache vyenye vitamin D, Lakini kwa kiasi kidogo unaweza kuipata kwenye peanut, yogurt, egg yorks na samaki.
Vyakula vyenye Omega 3s/DHA
Kwa watu wazima omega 3s imesaidia sana ugonjwa wa moyo, vile vile kwa watoto inafaida kama hizo,Kwa umri wa mtoto mdogo husaidia kwa kiasi kikubwa kwenye upande wa kuwa na ubongo wenye afya na macho yenye kuona vizuri, Vyakula vilivyo na omega3s ya kutosha ni samaki aina ya salmon, na avocado
Vyakula vyenye Vitamini A,B,C na E
Hizi vitamins zote nne zinausaidia mwili kuanzia juu mpaka chini, kwa kuweza kuwa na ubongo wenye afya atimaye kuwa na akili timamu, Kuwa na macho yanayoona vizuri,Ngozi inayongaa vizuri, Siri ya kuzipata hizi vitamamini kwenye chakuala cha mtoto pendelea kutumia vyakula kama, caroti, viazi vitamu hivi vina kiwango kikubwa cha vitamin A, Mboga za majani za kijani, ndizi, na maharage zina vitamin B, Nyanya, strawberries , zina Vitamini C, na mahindi, mchele zinavitamini E. Hivyo basi akina mama kwa kuandaa vyakula vya watoto tuzingatie hayo.
NI JUKUMU LA KILA MWANA MAMA KUMPATIA MTOTO WAKE LISHE BORA NA MALEZI MEMA.
No comments:
Post a Comment