Sunday, 21 April 2013

TAMADUNI YENYE NGUVU ILIYOBAKI AFRIKA KUTOKA TANZANIA.unaijua soma hapa..................

ERO SUVAI, KOKO TAKWENYA, KAANABO,KEYIAA, HIZI NI BAADHI YA SALAMU ZA KABILA LA KIMASAI , KABILA LINALOPATIKANA NCHINI TANZANIA HASA MKOANI ARUSHA NA BAADHI YA MAENEO MENGINE YA AFRIKA, MAASAI NI KABILA LINALOISHI KWA UFUGAJI ,KIASI KIKUBWA CHA CHAKULA NI NYAMA INAYOTOKAN NA WANYAMA KAMA NG"OMBE, MBUZI, NA KONDOO, KUNA MARIKA MBALIMBALI KMA MORANI,NGAYONI,,MAKAA,KORIANGA,LAMEJOK",



MORANI NI RIKA LA VIJANA WALIOINGIA JANDONI NA HILI NI RIKA AMBALO HUWA WALINZI WA MALI NA FAMILIYA WAKIWA NI WATU WENYE MAFUNZO YA MILA NA HESHIMA KUTOKA JANDO, MAASAI HUPENDA NYAMA NA DAMU ZADI NA HAPA NI NI NG"OMBE ANAPIGWA MKUKI WA SHINGO KUTOA DAMU AMBAYO NI SEHEMU YA CHAKULA KWA WAMASAI, DAMU HII HUWA MAHUSUSI KWA VIJANA WALIOKO JANDO KWAAJILI YA KUIMARISHA AFYA ZAO. 



KABILA HILI HUISHI KATIKA NYMBA ZA KITAMADUNI AMBAZO HUJENNGWA KWAUDONGO NA UMBO LA DUARA NA KUEZEKWA KWA NYASI KAVU, VIJANA WA KIMASAI WAKIWA MBELE YA NYUMBA YA KUISHI, PIA MAASAI UJUIKANA ZAIDI KUTOKANA NA MAVAZI YAO AMBAYO NI MASHUKA YANYE MCHANGANYIKO MZURI WA RANGI, SHUKA HIZI HUITWA RUBEGA AMA MGORORI.



VIJANA WA KIMASAI KATIKA RIKA LA SKOLIO AU NYANGULO, USONI HUJIPAKA MAJIVU AU LOKARIA AMBAZO NI MAPAMBO YA KITAMADUNI WANAYOJIPAKA WAKATI WA KUTOKA JANDONI,


 
VIJANA WA KIMASAI HUNGOJWA WAKUWE NDIPO WAINGIZWE JANDONI NA HII NI KWASABABU MORANI NI WALINZI WA JAMII NZIMA YA KIMASAI HIVYO JANDO INAHUSISHA MAADILI YA KIMILA NA HESHIMA AMBAYO HUTOLEWA KAMA MAFUZO KIPINDI CHA JANDO.NA HAPA NI VIJANA WA KIMASAI WAKIWA KATIKA SHEREHE ZA JANDO AMBAZO HUWA HIVI, NGAYONI AMBAYE NI KIJANA ANAYEINGIZWA JANDO HUVALISHWA BLANGETI FIMBO MKONONI NA MORANI WENGINE WANAKUWA WAMEMZUNGUKA HUKU WANAWAIMBIA NYIMBO ZENYE MAFUNZO YA JANDO KATIKA UJUMBE WAKE, SHEREHE ZA JANDO HUUSISHA WATU WENGI NA BAADA YA NYIMBO MORANI PAMOJA NA NGAYONI WANAELEKEA PORINI KWA USIKU MZIMA AMBAKO MAFUNDISHO YA UTU UZIMA HUTOLEWA PAMOJA NA MAELEKEZO MENGINE YA MILA

 

BASI SIKU ZA SHEREHE ZA JANDO MAASAI HUCHINJA NA KULA NYAMA KAMA SEHEMU YA KUFURAHI, WAZEE WAMAMA WATOTO NA WANADADA HUBAKI NYUMBANI WAKATI MURANI WANAONDOKA NA KWENDA PORINI, HUKAA PORINI USIKU MZIMA NA KURUDI NYMBANI SAA KUMI USIKU AMBAKO WATU HULA NYAMA NA KUIMBA MPAKA KUNAPOKARIBIA KUKUCHA NA HAPO NGAYONI HUPELEKWA MTONI KUOGA NA BAADA YA HAPO KITENDO CHA JANDO HUFANYIKA BILA GANZI.. MDA WA KUKAA JANDO NI MWEZI MMOJA AU ZAIDI.
 

WAKATI WA JANDO NGOZI YA NG"OMBE HUTUMIKA KAMA KITI CHA KUKALIA KWA ANAYAFANYIWA JANDO. HESHIMA, UTIIFU, UCHAPAJI KAZI , ULINZI WA JAMII NI MABO YANAFUNDISHWA JANDONI NA HII IKIMAANISHA KATIKA KABILA LA KIMASAI MORANI NI MTU WA KUHESHIMIKA SANA KUTOKANA NA YALE ALIYONAYO KWA JAMII NA FAMILIYA. MAASAI HUPENDA LOSHORO AMBAYO HUPIKWA NA MAHINDI NA MAZIWA, MAASAI HUIMBA NA KURUKA JUU NA HATA MDA MWINGINE KUZIRAI KUTOKANA NA FURAHA AMBAYO HUITWA MORI...HILO NI KABILA LA MAASAI UPANDE WA WANAUME SAHEMU YA PILI YA MAELEZO HAYA YATAENDA KUKUELEZEA BINTI WA KIMASAI ALIVYO KIMILA NA ANAVYOISHI.


No comments:

Post a Comment