Friday 3 May 2013

Kaburu: Kocha wa Simba ana roho ya Paka...........


Kocha Mkuu wa Simba Patrick Liewing (kushoto) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa timu hiyo Zacharia Hans Poppe,


BAADA ya klabu ya Simba kushindwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Godfrey Nyange Kaburu amesema Kocha Mkuu wa timu hiyo Mfaransa Patrick Liewing ana roho ya paka 
Akizungumza na Waandishi wa habari Kaburu alisema Kocha wa timu hiyo ana roho ngumu kama ya Paka ndiyo maana ameweza kufanya maamuzi magumu ya kuachana na wachezaji wakongwe na kutumia vijana huku akijua kwamba Simba inahitaji ubingwa.
"Patrick Liewing ni kocha mwenye kujua misingi ya kazi yake, ndiyo maana aliamua kuwatumia vijana wengi kutoka timu B ya Simba baada ya kuona wachezaji wakubwa wamejaa viburi na kuingia kwenye makundi ya baadhi ya viongozi"alisema Kaburi na kuongeza:
Pamoja na kwamba Simba ilikuwa katika wakati mgumu wa kutafuta Ubingwa wa LIgi Kuu huku pia ikiwa na migogoro ya uongozi, na kelele za mashabiki, lakini bado Kocha hakuangalia hilo badala yake akaweka nguvu kubwa katika kuandaa timu itakayoweza kuiletea Simba heshima katika msimu ujao wa Ligi".
Kaburu ambaye alijiuzuru nafasi yake ya uongozi katika Klabu hiyo alisema kwamba, vijana hao wamekaa pamoja kwa zaidi ya miaka 4 sasa na lengo kubwa ilikuwa ni kuwaandaa kwa ajili ya kuja kuisaidia timu katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment