Baadhi ya magari ya mizigo yakiwa yameegeshwa katika moja ya vituo vilivyopo kandokando ya Barabara Dar es Salaam- Morogoro yakisubiri kuendelea na safari
Ni kweli hapa wapo kina dada, ukiwataka mnaelewana tu. Mimi mwenyewe ninaye binti yangu ila nimetuma dukani, labda umsubiri. Lakini kama unaona utachelewa, basi nenda baa ya jirani hapo wapo wengi tu,” alisema mama huyo.
Licha ya kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya
Ukimwi, Mkoa wa Mbeya bado unatajwa kuwa eneo lililokithiri kwa vitendo
vya ngono bila kuwa na tahadhari (ngono zembe).
Dar es Salaam. Sababu kubwa ya
hali hiyo inaelezwa kuwa ni kuwepo kwa maegesho ya malori ya mizigo
yanayoelekea Zambia huku madereva wake wakitajwa kuwa wateja wakubwa wa
ngono.
Uchunguzi uliofanywa na Waandishi wa habari katika
maeneo yanayotajwa kwa biashara ya ngono yaani Kata ya Igawa na Igurusi,
umethibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo.
Igawa
Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa madereva wa taxi eneo la Igawa aliyejitambulisha kwa jina la Felix, alisema kuwa kwa sasa biashara hiyo imedorora kwa sababu madereva wa malori wamepunguza kusimama hapo.

“Zamani ungefika hapa saa hizi ungewakuta
barabarani kabisa. Lakini siku hizi, malori yameacha kusimama hapa,
ndiyo maana nao wamepungua. Lakini wapo baadhi yao ni wahudumu wa baa,”
alisema dereva huyo.
Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda na usafiri usiku ni wa shida, mwandishi aliendelea Kata ya Igurusi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Igurusi
Ni majira ya saa mbili usiku, baada ya kuchukua chumba kwenye nyumba ya wageni iliyo mbali na barabara kuu, nikarudi kwenye baa moja. Kabla sijaondoka, nikamuuliza mama mwenye gesti kama naweza kuleta mwanamke wa kulala naye. Akanijibu kuwa ni uamuzi wangu kwani haizuiwi.

Nilipofika katika baa moja iliyo pembeni mwa
barabara (jina linahifadhiwa) nilikuwa nikipata kinywaji huku
nikiangalia jinsi ya kumpata mtu wa kuzungumza naye kwa kina.
Namjaribu mhudumu mmoja wa baa hiyo kwa kumtongoza, lakini akasema hawezi kutoka na mimi kwa kuwa bado yuko kazini.
Namjaribu mhudumu mmoja wa baa hiyo kwa kumtongoza, lakini akasema hawezi kutoka na mimi kwa kuwa bado yuko kazini.
Nahamia baa nyingine ng’ambo ya barabara kwa lengo
hilohilo. Hapo nakutana na mama mmoja wa makamo, kisha kumweleza shida
yangu kwamba natafuta mwanamke wa kulala naye usiku huo.
“Ni kweli hapa wapo kina dada, ukiwataka
mnaelewana tu. Mimi mwenyewe ninaye binti yangu ila nimetuma dukani,
labda umsubiri. Lakini kama unaona utachelewa, basi nenda baa ya jirani
hapo wapo wengi tu,” alisema mama huyo.
Nikaamua kwenda kwenye baa hiyo jirani na hapo
nawakuta kina dada wapatao watano, huku wateja wakiwa wachache tu.
Nikaagiza soda na kuanza kuinywa taratibu. Bila kupoteza muda
nikamuuliza dada aliyeniletea soda (jina linahifadhiwa) kama naweza
kupata mshichana wa kulala naye usiku huo. Mahojiano yetu yakawa hivi
Mhudumu: Hapa wapo wengi tu… wote unaowaona hapa ndiyo kazi zao, sijui unamtaka nani?
Mwandishi: Mimi nakutaka wewe..
Mwandishi: Mimi nakutaka wewe..
No comments:
Post a Comment