Thursday, 2 May 2013

Wapo baadhi ya wanaume hulia na kudondosha machozi katika mahusiano,,



Kilio cha mwanamume katika mahusiano,kinaweza kutokana na sababu mbalimbali ,,kusalitiwa,kukataliwa penzi, kudanganywa na baadhi ya wanawake,utakuta mwanamume amemsomesha mwanamke kuanzia Sekondari hadi chuo,lakini mwanamke baada ya kupata kazi anaolewa na mtu tofauti,ni kitendo ambacho kinaumiza sana kwa yule aliyetendewa,ndio maana hata baadhi ya wanaume hujikuta hawana mapenzi ya dhati tena kutokana na kutendwa.



Katika kulia hali hii huwa inatofautiana,kuna yule ambaye atalia kwa uchungu kutokana na mabaya aliyotendewa huku moyoni akiwaza namna ambavyo atalipiza kisasi,na hii huwa mbaya zaidi.kulia katika mahusiano haiangalii mwanamke au mwanamume,ijapokuwa maumivu yanatofautiana..na kuna baadhi ya watu hudiriki kusema wanaume huwa hawaumii sana kama wanawake,,mmmh ,,sijui mnalizungumziaje hili wadau............

No comments:

Post a Comment