Zifuatazo ni nukuu za maneno yaliyotolewa na Waziri wa nchi
Ofisi ya Rais, sera, uratibu na bunge William Lukuvi kuhusu hilo bomu
ambalo lililipuliwa kwenye mkutano cha Chadema Arusha.
“Mtu asiejulikana alirusha kitu katika kundi la watu
kilichosababisha mlipuko mkubwa, mkutano huu ulikua na ulinzi wa jeshi
la Polisi wakiwa na magari mawili… askari walisimama upande wa Kaskazini
ya uwanja ambapo mrushaji alikua mashariki na alirusha bomu kuelekea
Magharibi”
“Jaribio la Askari Polisi kutaka kumfata alierusha lilizuiwa
na makundi ya Wananchi ambao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe na
kuwazomea na hivyo Polisi kulazimika kuanza kujiokoa badala ya kumsaka
Muhalifu”
“Mlipuko huo ulisababisha watu wawili kufariki dunia ambao ni
Judith William (48) na mtoto Ramadhan Juma (15) na watu 70 wamejeruhiwa
miongoni mwao watatu wamejeruhiwa vibaya na wawili hali zao ni mbaya”
“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mlipuko huo ulikuwa ni wa
bomu la kurusha kwa mkono ambapo pia aina ya urushaji wa bomu hilo
haitofautiani na mbinu iliyotumika kwenye shambulio jingine la bomu
lililotokea kwenye kanisa la Olasiti Arusha”
“Kutokana na mfululizo wa matukio haya mageni, Serikali
imeamua kutenga shilingi milioni 100 kama zawadi kwa mtu yeyote
atakaeshirikiana na kutoa taarifa zitakazofanikisha kunaswa kwa muhalifu
wa matukio ya aina hii na mtandao wake mzima”
No comments:
Post a Comment