BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje
kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua
barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa
bodaboda.
Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo
cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es
Salaam.
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari
wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake
halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa
muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na
kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume .
Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.
Mara baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na
uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa
teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na
ubovu wa barabara.
“Hali ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye
alifika na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli
yake,” alisema Josephine kwa uchangamfu.
Binti huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.
Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.
Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.
Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.
No comments:
Post a Comment