Tuesday, 18 June 2013
Sugu anusurika kufa,gari la Tundu Lissu lapigwa bomu
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ameusurika kufa wakati akielekea Jijini Arusha kuwahi kuaga miili ya marehemu waliouawa kwa mabomu yaliyolipuliwa siku chache zilizopita kwenye mkutano wa Chadema jijini hapa.
Joseph Mbilinyi aliamua kwenda kuungana na Wananchi wa Arusha na wanachama wa Chadema, amepata ajali hiyo maeneo ya Kateshi Wilaya ya Hanang.
Ajali hiyo imetokea baada ya gari la Mbunge huyo kugongana na gari la abiria lililokuwa katika mwendo kasi,na katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa zaidi ya gari la mbunge huyo kuharibika vibaya.
Mbali na Gari Sugu kuahribika vibaya taarifa kutoka Arusha pia inaeleza kwamba Gari la Tundu Lissu pia limepigwa bomu kama ilivyokuwa gari la Lema.jijini Arusha hali bado si shwari kwani Askari Polisi wanaendelea kutawanya waandamanaji walioamua kuingia mitaani huku wakiwa na mji kwenye madumu kwa ajili ya kuwa kila wanapopigwa mabomu na Polisi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment