Ni vigumu kufahamu haya, lakini ndio ukweli kuwa kuna kasi ya kuongezeka kwa wanaume dhaifu nchini na ulimwengu kwa ujumla.
Kulingana na taarifa za Shirika la Afya Duniani
(WHO), tatizo hili la wanaume dhaifu linaongezeka kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo kuendekeza ulevi, matumizi ya tumbaku/sigara,
kutokula kwa kuzingatia mchanganyiko wa vyakula (ulaji usiofaa) na watu
kutopenda mazoezi.
Hapa nchini hakuna utafiti thabiti uliofanywa
lakini nafikiri tutakubaliana kuwa tatizo hili lipo tena ni kubwa, kwani
kinyume na hilo kusingekuwa na watu wengi wanaojitangaza kwamba
wanatibu. Marekani wamefanya utafiti, Shirika liitwalo National
Ambulatory Medical Care Survey (NAMCS) ambalo linasifika kwa kufanya
tafiti mbalimbali za masuala ya afya, linasema kwamba ukionana na
Wamarekani 1,000 ujue kwamba 22 ni wanaume dhaifu.
NAMCS ikasema pia kwamba zaidi ya wanaume milioni
2.6 wanatumia dawa za kuongeza nguvu; ndio nasema kwamba sisi Tanzania
hatujafanya utafiti rasmi uliotangazwa na Serikali, lakini wewe bila
shaka utakuwa shahidi kwamba ziko dalili kwamba hali ni mbaya.
Kuna mtafiti mmoja maarufu kutoka India, Dk Srini
Vasakumar, kutoka kituo cha utafiti wa tiba kiitwacho Institute of
Biology and Clinical, India, ambaye amekuwa akitoa huduma za kuponya
tatizo hilo la udhaifu katika maeneo mbalimbali hapa nchini, anasema
hili ni tatizo linaloweza kupona, shida ya wengi ni kutochukua hatua;
wengi wanalia, badala ya kuchukua hatua.
Daktari huyo mwenye Shahada ya pili ya Tiba kwa
kutumia vyakula na Shahada ya uzamivu ya tiba kwa ujumla, anasema wengi
wanaendelea kuwa na tatizo hili kwa kutochukua hatua thabiti; wengi
wamesoma na wanafahamu kuna aina za vyakula vinasaidia wanga, nguvu,
mafuta na vitamini... lakini wanakula ili mradi tumbo lijae.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha
Mapinduzi, Janet Bina Kahama, Aprili 10, mwaka 2007 katika kikao cha
saba cha Bunge aliuliza swali namba 8 (b); je, Serikali inafahamu ni
sababu gani zinasababisha kupungua kwa nguvu za kiume kunakotangazwa
sana na waganga wa jadi?
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa alijibu kuwa tatizo hili linasababishwa na mambo mengi, baadhi yao ni lishe duni hasa mboga za majani, kutokula aina mbalimbali za jamii ya karanga, matumizi yasiyofaa ya ulevi kama pombe.
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa alijibu kuwa tatizo hili linasababishwa na mambo mengi, baadhi yao ni lishe duni hasa mboga za majani, kutokula aina mbalimbali za jamii ya karanga, matumizi yasiyofaa ya ulevi kama pombe.
Sababu nyingine ni matumizi ya sigara, dawa za
kulevya, dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa kama kisukari, shinikizo la
damu, magonjwa ya akili na kutopumzika kunakosababishwa na shughuli
nyingi za kijamii hivyo kusababisha uchovu.
Kwa uzoefu wangu kama mtu ambaye nimekuwa nikitoa
ushauri kuhusu masuala ya ndoa ni kwamba tatizo hili lina athari kubwa
katika ndoa, baadhi ya wanawake sasa hawaangalii uzuri wa mwanaume, wala
utajiri au elimu yake ama tabia, kwanza wanatamani kujua kama mume
mtarajiwa ni mume dhaifu au la.
Athari za kuwa dhaifu ni kwamba baadhi ya wanawake
unaweza kumpa mamilioni ya fedha, magari nk lakini unachohonga akaenda
kuhongwa mwingine. Unamnunulia gari, unaweza kushangaa unakutana naye
anatembea kwa miguu, gari kapewa kijana atanue nalo.
Ninachotaka kusema ni kwamba kila wanaume kuchukua
tahadhari juu ya jambo hili ambalo linaonekana wazi kuwakwaza wanawake
wengi kiasi cha baadhi kuamua kuvunja uhusiano. Hata hivyo kama mwenzi
wako ana tatizo ni vizuri kuangalia namna ya kulitibu, sio kukimbiana,
kwani hakupenda kuwa hivyo.
No comments:
Post a Comment