Friday, 16 August 2013

KWA WALE WOTE WANAOPENDA KUWASUKA WATOTO WADOGO NA KUWAWEKEA DAWA ZA NYWELE, NI MBAYA KUKOMAZA UBONGO WA MWANAO!


MTOTO kisheria ni binadamu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18. Maana ya kutambua  hilo inaonekana pale jamii inapozingatia malezi na makuzi sitahili kwake, katika nyanja mbalimbali za maisha ili anapofikia umri unaomuwezesha kuweza kupambanua mambo, ajiweke mbali na hatari nyingi zinazowapata watu kutokana na historia ya malezi na makuzi yao.

Bila shaka kila mtu anatambua umuhimu wa kutunza afya ya binadamu na kwamba jambo hilo hutakiwa kuanza tangu mtoto akiwa tumboni mwa mama yake.

Usafi wa mwili ni miongoni mwa mambo yanayotakiwa kuzingatiwa na kila mtu, kwa kuwa mtoto hawezi kujitunza kazi hiyo hutakiwa kufanywa na mzazi au mlezi huku akimfunza hatua kwa hatua, kwa kuzingatia umri na uwezo wa akili wa mtoto husika.

Usafi wa mwili ni dhana pana kwani unahusisha hata kumkinga mtoto na matumizi ya bidhaa zenye kemikali zenye hatari kwa afya yake ambazo matokeo yake yanaonekana mara baada ya matumizi ya bidhaa hizo au baada ya muda mrefu kupita.

Baadhi ya watu, hususani wanawake wamekuwa na kasumba ya kuwaruhusu au kuwawekea watoto dawa kwenye nywele kwa lengo la kuzifanya ziwe laini. Jambo hili si jema kwani madhara yake ni makubwa ambayo matokea yanaonekana baada ya miaka mingi, tangu muhusika atumie dawa hizo.

Dawa nyingi za kulainisha nywele mathalani relaxer zina kemikali ya Zebaki, ambayo wataalamu wa afya wanasema inapotumiwa kwa muda mrefu inaathiri mishipa iliyo kwenye mfumo wa uzazi.

Mfumo wa uzazi unapoathiriwa na kemikali ya Zebaki, mishipa iliyo kwenye mfumo huo inalegea na kusababisha mwamamke husika kushindwa kushika mimba au kushika mimba ambazo uharibika.

Hata kwa mwanawake mwenye umri pevu ambaye bado anahitaji la kupata watoto dawa hizi ni hatari ingawa kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na ilivyo kwa mtoto. Ili kuepuka hatari hizo, inashauriwa mtumiaji wa dawa hizo kuzingatia mashari ya matumizi ya dawa hizo hususani muda.

Kwa kawaida inashauriwa mtu mzima kuweka dawa kwenye nywele siyo zaidi ya mara nne ndani ya mwaka mmoja. Unapoweka dawa unatakiwa usirudie mpaka miezi mitatu ipite, tofauti na hivyo unahatarisha afya yako.

Ipo dhana kwamba siku hizi kuna dawa maalumu kwa ajili ya watoto, lakini ikumbukwe kuwa nazo zina kemikali hivyo ili kuzingatia umuhimu wa afya ya mtoto ni bora kuacha kutumia dawa hizo na badala yake kutunza usafi wa mwili na mavazi ya mtoto ili awe na mwonekano nadhifu usiyo na madhara.

Mtoto anaweza kuwa na mwonekano mzuri wa kupendeza akiachwa mwenye katika hali yake ya asili. Wazazi warejee nyendo zao, wakague utekelezaji wa majukumu yao kwa familia hususani yale yanayogusa moja kwa moja malezi wa watoto kusudi madhara yasiyo ya lazima kwa watoto yadhibitiwe.

Hakuna mzazi anatakaye furahi mtoto wake akiolewa alafu akakosa mtoto, pia mtoto anapofahamishwa athari za matumizi ya dawa hizo inakuwa vizuri kwa sababu hata ikitokea akalazimika kuishi nje ya wazazi wake ataweza kuepuka matumizi ya dawa hizo, hata akiwa mtu mzima akaamua kuzitumia atazingatia masharti ya matumizi yake.

hivyo ni jukumu la wazazi kuchukua hatua za kuhakikisha afya za watoto wao haziathiriwi na mambo yanayoweza kuzuilika.

Siyo vizuri kuiga kila tunaloona bila kufuatilia na kubaini athari zinazoweza kutokea, kabla ya kutumia kitu ni vizuri kufanya utafiti na uamuzi wa kukitumia au kukiacha ufanywe baada ya kupima faida na hasara zake.
Wazazi wengi wamekuwa na tabia ya kuwasuka watoto mitindo mbali mbali wakidhani wanasaidia kuwapendezesha kumbe wanasaidia kukomaza ubongo wa mtoto kwa kuvutwa mishipa ya ngozi ya kichwa hivyo kumfanya mtoto akomae ngozi ya uso kabla y a wakati. Hiyo ni hatari kubwa sana kwa mtoto wako na madhara utayaona katika ukuaji wa mtoto.

No comments:

Post a Comment