Mwenyekiti wa Kamati hiyo ZITTO KABWE amesema kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa namba tano kifungu cha 14 kifungu kidogo cha kwanza B, ya mwaka 1992 vyama ya siasa vinapaswa kupeleka hesabu zao zilizokaguliwa kwa msajili wa vyama lakini kati ya mwaka 2009/2010 na mwaka 2012/2013 hakuna chama chochote kilichopeleka hesabu zake kwa Msajili wa vyama vya siasa.
Mwenyekiti huyo wa PAC ZITTO KABWE amesema badala ya vyama kufanya malumbano na kamati ya Bunge vinapaswa kuchukua hatua za kufuata sheria kwa kukagua hesabu zao kutokana na fedha zinazotolewa kwa vyama hivyo kama ruzuku kuwa ni za walipa kodi.
Mwishoni mwa wiki Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM NAPE NNAUYE alitoa tamko la kupinga taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamati ya Bunge ya PAC na kubainisha kuwa hesabu za chama chao huwa zinakaguliwa na kuwa wapo tayari kuwasilisha vielelezo mbele ya kama hiyo iwapo vitahitajika.
Tukisalia katika kamati za Bunge Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba Dk. PINDI CHANA ametoa wito kwa wananchi kuitumia Katiba ya sasa katika kupitia Rasimu ya Katiba mpya ili kufanya mlinganisho wa masuala mbalimbali.
Akizungumza wakati wa semina ya wabunge kuhusu masula ya Katiba PINDI amesema suala la Katiba linapaswa kutiliwa maanani hivyo kila mwananchi anapaswa kuisoma rasimu na kuilelewa hasa wale wenye dhamana ya kuwawakilisha wananchi katika Bunge la Katiba.
No comments:
Post a Comment